Theolojia Katika Picha

/ 1 7 9

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

Kusudi la maadili ni kuhakikisha kwamba theolojia yetu inaathiri tabia na mitazamo yetu. Hayaishii tu kutufanya tuielewe kweli. Badala yake, yanatafuta kila mara kutusaidia kugundua jinsi ya kuitumia kweli (na kujaribu kututia motisha kufanya hivyo). Tabia halisi ya kimaadili inamaanisha kuwa kanuni za kimaadili zinaeleweka, zinazingatiwa na kutumika katika hali na mazingira husika katika mchakato mzima wa kubuni mikakati na shughuli au mbinu mahususi. Katika shirika, tabia halisi ya kimaadili pia inadai kwamba mikakati na mbinu ambazo zimebuniwa zifanyiwe majaribio, tathmini na uboreshaji wa mara kwa mara. Hii inasaidia kuhakikisha kwamba shirika linatimiza kivitendo kile ambacho linadai linaamini kupitia ukiri na kanuni zake. Mwisho, ni lazima ieleweke kwamba uzoefu wetu daima hutufanya tukabiliane na vitendawili, hitilafu na vipaumbele vinavyoshindana. Maadili ya maendeleo hayajaribu kurahisisha maisha kwa kuyaweka katika mfumo mzuri. Badala yake, yanatoa kanuni ambazo zitatusaidia kutambua jambo lililo muhimu zaidi katika hali fulani mahususi inayotukabili. Kila uamuzi wa kimaadili lazima uhusishe majadiliano kuhusu jinsi kanuni mbalimbali zilizoainishwa hapa chini zinavyohusiana na kuhusu zipi ni maadili muhimu zaidi kwa uamuzi fulani. Ni katika mazungumzo tu na katika maombi ndipo uamuzi sahihi unaweza kutambuliwa. Kanuni za kimaadili za Ufalme wa Mungu zinaweza kudhihirishwa kupitia vigezo vya uhuru, ustawi na haki. Vigezo hivi ni shina na matunda ya kufanya maendeleo katika mtazamo wa Ufalme. Uhuru ni uwezo wa kutumia uwezo wetu tuliopewa na Mungu wa kufanya maamuzi yanayoakisi upendo. Kwa hiyo, maendeleo yanapaswa kuleta uhuru kwa kusaidia watu binafsi: • Kupata utu na heshima. • Kuwezeshwa kufanya maamuzi ya busara. • Kuwajibika kwa ajili ya maisha yao wenyewe na ya wengine. Mchakato huu unahusisha kuwasaidia watu kuelewa na kufikia kile wanachohitaji ili kuishi kwa uhuru katika jamii kama watumishi wa Ufalme wa Mungu wanaowajibika kibiblia, wanaojiongoza, na wanaoendelea kukua. Hili linamaanisha kukuza aina ya mahusiano ambayo si ya utegemezi wala ya kujitegemea kama mtu aliye kamilika na asiyehitaji wengine, bali mahusiano ya kutegemeana kwa upendo ambayo yanaweza kuzaa ushirikiano, kuheshimiana, na kuongezeka kwa wigo wa uhuru.

6. Kazi ya Maendeleo ya World Impact Inazingatia Msingi wa Uhuru

Made with FlippingBook Digital Publishing Software