Theolojia Katika Picha

1 7 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

• Kutoa Kielelezo cha Matokeo ya Injili Hatuwezi kutegemea kuzalisha makanisa yenye nia ya dhati ya kushiriki katika kazi ambayo hawajawahi kuona ikitekelezwa kwa vitendo. Tunashiriki katika kazi ya maendeleo kwa sababu tunatarajia makanisa mapya yaliyopandwa kufanya vivyo hivyo. Tunataka kutoa mfano hai kwamba Injili lazima ichukue hatua kutoka imani hadi matokeo yaliyo dhahiri, kutoka neno hadi tendo. 4.2 Kumbusho Muhimu Kuna tahadhari hii muhimu ya kuzingatia. Hatuwezi, kwa juhudi zetu wenyewe, kuuleta Ufalme wa Mungu. Kama vile Paul Hiebert anavyotukumbusha, “Mielekeo yetu itakuwa na dosari ikiwa tutaanza kazi ya umisheni kwa shughuli za kibinadamu. Utume kimsingi sio kile tunachofanya. Ni kile ambacho Mungu anafanya” (Hiebert 1993, 158). Uinjilisti, upandaji makanisa na maendeleo, vyote hufanya kazi, kwanza kabisa, chini ya maongozi na mamlaka ya Roho wa Mungu. Kujua nini kifanyike, na jinsi tunavyopaswa kufanya, kamwe hakuamuliwi kupitia michoro ya kimkakati au mbinu ambazo mashirika yamezifanyia utafiti na kuzithibitisha. Wajibu wetu wa kwanza ni kuwa waaminifu kwa Mfalme, kusikiliza maagizo yake na kuitikia mipango yake. Tumeeleza kuwa: Watendakakazi wa maendeleo wanatakiwa kuwezesha watu binafsi, makanisa na makundi katika jamii kupiga hatua kuelekea uhuru, ustawi, na haki ya Ufalme wa Mungu. Mchakato unaotupeleka kwenye kusudi hili, na maamuzi tunayofanya ili kufikia malengo haya lazima viongozwe na maadili ambayo yanapatana na viwango vya Mungu kwa habari ya mahusiano ya kibinadamu. Maadili yanahusiana na mwenendo na tabia ya mwanadamu. Ni uchunguzi yakinifu wa kanuni na mbinu za kutofautisha mema na mabaya, yanayofaa na yasiyofaa. Maadili ya Kikristo ya maendeleo hutusaidia kufanya maamuzi kuhusu masuala ya maendeleo kwa kuzingatia ufunuo wa Biblia na theolojia. Yanatuwezesha kufikiri na kutenda kwa uwazi ili tuweze kutambua lililo sawa na jinsi linavyopaswa kufanyika. Maadili ya Maendeleo

5. Utangulizi

Made with FlippingBook Digital Publishing Software