Theolojia Katika Picha
/ 1 7 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
uhusiano wa moja kwa moja na uinjilisti na upandaji na malezi ya makanisa yanayozaliwa. Shirika la kimisheni linathamini mashirika mengi ya maendeleo ambayo yanajihusisha na aina hii ya kazi. Ingawa shirika la kimisheni litataka kuwa na ubia na shirika la maendeleo (na kuomba kwamba Mungu aongeze idadi na ufanisi wa mashirika hayo kwa kiasi kikubwa), shirika la kimisheni lenyewe litazingatia miradi ya maendeleo inayosaidia kazi ya uinjilisti, ufuasi, na uanzishaji wa makanisa ya kienyeji. Pasipo kujipambanua huku kwa umahususi, shirika la kimisheni litapoteza uwezo wake wa kukamilisha sehemu yake katika kazi pana ya Mungu. 4.1 Tamko la Dhumuni Ingawa tunatambua uhalali wa kujihusisha katika kazi za maendeleo kama mwitikio wa moja kwa moja wa kimungu kwa mahitaji ya binadamu, tunaamini kwamba tumeitwa kujikita katika kazi za maendeleo ambazo hasa zinasaidia na kuchangia katika kazi ya uinjilisti, ufuasi na upandaji makanisa. Kwa kuzingatia hili, tunapambanua msimao wetu kama ifuatavyo. Lengo la huduma za maendeleo za World Impact ni kusaidia uinjilisti, uanafunzi, na malengo ya World Impact ya upandaji makanisa kwa: • Kuonyesha Upendo wa Kristo Watu wengi waliokandamizwa wana msingi mdogo wa kuelewa upendo wa Mungu kwao na haki na huruma ambavyo ni kiini cha asili na tabia yake. Kazi ya maendeleo inaweza kutoa ushuhuda hai wa upendo wa Kristo na namna anavyojali uwepo wa haki na amani katika mitaa ya majiji. Huduma inayolenga kugusa maisha ya mtu katika ujumla wake inaweza kufanyika sanjari na utangazaji wa Injili kwa maneno, kuthibitisha uhalisia wake na kuimarisha kina cha uelewa miongoni mwa wasikilizaji wake. Shughuli ya maendeleo inaweza kufanya kazi kabla ya uinjilisti ili kuwaandaa watu kusikiliza kwa dhati maneno ya Kristo na ujumbe wake wa wokovu. • Kuyawezesha Makanisa Yanayochipukia Makanisa yanayochipukia mijini mara nyingi yana rasilimali chache za kimwili zinazoweza kutumika kukabiliana na mahitaji makubwa ya majiji. Taasisi ya maendeleo ya kikristo inaweza kushirikiana na wachungaji wa makanisa yaliyopandwa, ili kutoa fursa za upatikanaji wa rasilimali na programu ambazo zinaweza kukidhi mahitaji ya msingi ndani ya makusanyiko yao, kuhimiza maendeleo ya uongozi, na kusaidia makusanyiko yao kushiriki katika kuifikia jamii yao kwa namna inayohudumia mahitaji ya watu kiroho na kimwili.
4. Kazi za Maendeleo ndani ya Wakala Wetu wa Umisheni
Made with FlippingBook Digital Publishing Software