Theolojia Katika Picha
1 7 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo”. Vipengele hivi vinaweza kufupishwa kama “uhusiano wenye sura tatu kati ya uinjilisti na shughuli za kijamii. Kwanza, shughuli za kijamii za Kikristo [maendeleo] ni matokeo ya uinjilisti, kwa kuwa wanaojihusisha nazo ni watu waliokwisha ipokea Injili. Pili, shughuli za kijamii za Kikristo ni daraja la uinjilisti, kwa kuwa zinadhihirisha upendo wa Mungu na hivyo hushinda ubaguzi na kufungua milango iliyofungwa. Tatu, ni mshirika wa uinjilisti, kwa namna ambavyo zinafanya kazi ‘kama visu viwili vya mkasi au mbawa mbili za ndege’” (Stott 1995, 52). 3.3 Haja ya Umahususi Utume wa kisasa umeshuhudia ongezeko kubwa la mashirika ya kimisheni na ya maendeleo. Hili hutokea pale mashirika yanapojikita na kubobea katika eneo moja mahususi la kazi kubwa na pana ambayo Mungu ameitoa. Utambuzi huu wa hitaji la umahususi uliibuka mapema katika maisha ya Kanisa. J. Chongham Cho anatoa maoni yafuatayo: Katika Matendo 6 . . . kulifanyika utofautishaji kati ya uinjilisti na huduma za kijamii. Jambo hili halikuwa mgawanyiko kimsingi bali lilifanyika kwa ajili ya kuleta ufanisi wa kiutendaji katika utume wa kanisa na kama suluhisho la tatizo lililotokea katika kanisa. Hili ni tendo linaloakisi tafsiri muhimu ya asili ya kanisa kama mwili wa Kristo. Ingawa tunapaswa kupinga utenganishaji hasi kati ya uinjilisti na huduma za kijamii, hatupaswi kupinga umahususi (Cho 1985, 229). Kama taasisi ya kimisheni, lengo letu kuu ni uinjilisti na ufuasi ambao unasababisha upandaji wa makanisa ya kienyeji. Ukweli kwamba uinjilisti, upandaji makanisa na maendeleo vimeunganishwa una maana kwamba mashirika ya kimisheni, hasa yale yanayowalenga watu maskini na wale wanaokandamizwa, yatashiriki katika aina fulani ya kazi za maendeleo. Hata hivyo, shirika la kimisheni lazima liwe makini katika kubuni kazi zake za maendeleo ili kazi hizo ziweze kuchochea kazi kuu ya uinjilisti na upandaji makanisa badala ya kuidhoofisha. 4 Tunapaswa kushiriki katika kazi ya maendeleo ambayo inakuza uanzishaji, afya, ukuaji, na uzidishaji wa makanisa ya kienyeji miongoni mwa jamii maskini. Umahususi unaruhusu mashirika kuongeza mafunzo na rasilimali ambazo zinaweza kutengwa na kuelekezwa katika eneo maalum la kazi kubwa ya umisheni. Taasisi ya maendeleo inaweza kujihusisha katika miradi mingi mizuri na muhimu ambayo haina
4 Tazama Kiambatisho A kupata mitazamo mbalimbali kuhusu jinsi kazi
ya maendeleo isiyotekelezwa
ipasavyo inavyoweza kuathiri vibaya kazi ya umisheni.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software