Theolojia Katika Picha

/ 1 7 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

3.2 Kutegemeana na Kuunganishwa Uhusiano kati ya kazi ya Umisheni na Maendeleo ni mtambuka. Kuunganishwa huku kuna mambo mengi. • Zimeunganishwa na lengo moja. Wamishenari kadhalika watendakazi wa maendeleo hawaridhiki hadi upatanisho kati yaMungunamwanadamuna upatanisho kati yamwanadamunamwanadamu umefikiwa kabisa. Tunaamini kwamba hili linafanya umisheni na maendeleo kuwa shughuli zenye msingi wake ndani ya Kristo kwa maana ya mwelekeo, kwa kuwa ni “ndani ya Kristo” ambapo Mungu anaupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Kristo ndiye Mfalme. Ni kifo chake cha kujidhabihu, cha upatanisho ambacho kinatoa msingi wa kusudi la upatanisho kati ya wanadamu na Mungu, na ndani ya mahusiano na mifumo ya maisha ya kibinadamu. Ni mamlaka na uwepo wake wa kifalme vinavyowezesha Ufalme kuingia katika enzi hii ya sasa na kuharibu kazi za giza na kuunda jumuiya za kweli zilizokusanywa chini ya utawala wa Mungu. • Zinahifadhi kiwango fulani cha uhuru na kujitegemea. Shughuli za uinjilisti na kupanda makanisa wakati mwingine zinaweza kufanyika bila kuzingatia kazi ya maendeleo. Kadhalika, kazi ya maendeleo wakati mwingine inaweza kufanyika bila kuambatana na shughuli ya upandaji kanisa. Kwa sababu zote mbili ni mwitikio wa kweli kwa utendaji wa Mungu ulimwenguni, zinaweza, pale inapofaa, kufanya kazi kwa kujitegemea. Ingawa kila moja ni shughuli halali inayojitegemea yenyewe, ni wazi kwamba litakuwa jambo lenye afya na la kawaida zaidi pale ambapo shughuli hizi mbili zinafanyika pamoja. • Zinahitajiana kwa ajili ya ufanisi wa kudumu. Bila uinjilisti, hakuna maisha yaliyobadilika, hakuna wapatanishi wanaoelewa mpango wa Mungu kwa mwanadamu na jamii na ambao wanaleta mabadiliko kwa nguvu za Roho. Bila maendeleo, makanisa yaliyoanzishwa na umisheni yanajitenga, na hayafanyi kazi kama “chumvi na nuru” katika jamii zinazoyazunguka na katika taifa. Juhudi za kimishenari hudhoofishwa wakati ambapo kanisa lililopo haliwezi kufanya athari za utawala wa ufalme wa Mungu zionekane kupitia maisha ya kanisa hilo. Kuunganishwa kwa mambo hayo mawili kunaonyeshwa ipasavyo katika Waefeso 2:8-10 inayosema, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana

Made with FlippingBook Digital Publishing Software