Theolojia Katika Picha

1 7 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

Kwa hiyo, tunasisitiza kwamba: Watendakakazi wa maendeleo wanatakiwa kuwawezesha watu binafsi, makanisa na makundi katika jamii kupiga hatua kuelekea uhuru, ustawi, na haki ya Ufalme wa Mungu.

2.3 Kiunganishi cha Pamoja Wamishenari na watendakazi wa Kikristo wa maendeleo wameunganishwa katika kujitolea kwao kwa pamoja kuendeleza utawala wa ufalme wa Mungu katika nyanja zote za maisha. Shughuli ya umishenari inahusu kutangaza “habari njema” inayowaita watu kuingia katika Ufalme wa Mungu kupitia tendo la wokovu na kuzaliwa upya. Inalenga katika kuwaleta katika jamii ya waliokombolewa, watu, tamaduni, na makundi ya watu ndani ya tamaduni ambazo hazijafikiwa (yaani, “kuuleta ulimwengu katika Kanisa”). Hayo yote yanafanywa kwa lengo la kuanzisha makanisa ambayo yanaweza kuwafanya washirika wao watambue utawala wa Mungu na kuishi kulingana na maadili ya Ufalme wake katika maisha yao binafsi na katika maisha ya ushirika (jumuiya). Shughuli ya umishenari pia inajumuisha maendeleo ambayo yanalenga kuita kila eneo la maisha kupatana na utawala wa ufalme wa Mungu. Inatathmini kila hali halisi ya maisha kwa msingi wa Sala ya Bwana (“Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni”) na kujihusisha katika matendo mema, upendo, na haki ambayo yanaonyesha asili ya mpango wa Mungu kwa watu wote. Inalenga kuleta utawala wa Mungu katika kila uhusiano na mfumo wa maisha ya wanadamu (yaani, “kulipeleka Kanisa ulimwenguni”). 3.1 Uhusiano wa Ubia Uinjilisti wa kimishenari na upandaji makanisa na kazi ya Kikristo ya maendeleo ni washirika katika mchakato wa kutangaza, kuonyesha na kupanua utawala wa Mfalme. Yote mawili ni mwitikio unaosababishwa na ukweli kwamba Mungu ametangaza nia yake ya kuupatanisha ulimwengu na nafsi yake kupitia zawadi ya Mwanawe. Ingawa kila moja ni mwitikio halali kwa mpango wa Mungu kwa ulimwengu, wala si mwitikio unaojitosheleza wenyewe. Maneno kadhalika na matendo ni sehemu muhimu katika jukumu la Kanisa la kutangaza Ufalme wa Mungu na uaminifu wake kwa Ufalme huo.

3. Uhusiano wa Kitheolojia kati ya Uinjilisti na Maendeleo

Made with FlippingBook Digital Publishing Software