Theolojia Katika Picha
/ 1 7 3
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
sababu hii misiolojia lazima ielekeze juhudi zake katika kudhihirishwa kwa wingi wa ishara zinazoonekana za Ufalme wa Mungu katika marefu na mapana ya sayari hii (Verkuyl 1993, 72-73). Uinjilisti, upandaji makanisa na maendeleo vinatokana na msingi mmoja wa kitheolojia: nia ya kuishi kwa kudhihirisha maana ya Ufalme wa Mungu ambao umeingia katika enzi hii ya sasa katika nafsi ya Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme. Ufalme huu upo tayari japo bado haujakamilika. Kwa sasa unasonga mbele kwa nguvu na kuenea kama chachu katika donge, lakini pia unangojea kurudi kwa Kristo wakati kila goti litakapopigwa na kutakapokuwa na mbingu mpya na nchi mpya. Kazi zetu za uinjilisti na za maendeleo zinatambua utawala wa kifalme wa Mungu, sasa, wakati ambapo ulimwengu kwa ujumla hautambui. Tunatangaza habari njema za Ufalme unaoenea wa amani na haki, tunawaita watu kwenye toba na wokovu kupitia imani katika Mfalme wake, tunalo tumaini la ushindi wake kamili usioepukika, na tunaishi kwa utii wa amri na maadili yake katika zama hizi. Kwa kuwa kazi ya uinjilisti/upandaji makanisa na kazi ya maendeleo zina uhusiano wa karibu, wale wanaojihusisha nazo mara nyingi hugundua kwamba majukumu yake na miradi yake vinaingiliana. Ingawa hili ni jambo la kawaida na zuri, kufafanua wazi kila jukumu tokea mwanzo kunaweza kusaidia kupunguza mkanganyiko ambao wakati mwingine unaweza kutokea katika mchakato huu.
2. Kazi ya Ufalme
2.1 Wamishenari Wamishenari wameitwa kuanzisha kazi mapya zinazolenga kuwafikia watu, matabaka ya kijamii, au vikundi vya kitamaduni katika maeneo ambayo hayajafikiwa (au ambayo
hayajafikiwa vizuri) na Injili. Kwa hiyo tunasisitiza kwamba:
Wamishenari wanatakiwa kuvuka mipaka ya kitamaduni ili kupeleka Injili na kufuasa vikundi ambavyo havijafikiwa kwa lengo la kuanzisha makanisa yanayojizidisha kati yao na kuyaingiza katika utumishi wa utawala wa Ufalme wa Mungu.
2.2 Watendakazi wa Maendeleo Watendakazi wa maendeleo wameitwa kukabiliana na hali na mifumo katika ulimwengu huu, ambayo haijitiishi chini ya utawala wa Mungu.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software