Theolojia Katika Picha

1 7 2 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

Akisimama katika mapokeo ya sheria ya Musa, anafafanua ujumbe wa msingi wa . . . manabii; Anakamilisha upatanisho kati ya ulimwengu na Mungu; Anafungua njia ya Ufalme wa sasa na ujao ambao unatudai maamuzi katika nyanja zote za maisha (Verkuyl 1993, 72).

1.3 Majukumu kwa Wale Wanaotafuta Ufalme wa Mungu Athari za Ufalme wa Mungu katika kazi ya utume zinaweza kuelezewa katika kweli tatu kuu. Theolojia inayozingatia Ufalme na misiolojia itajikita katika: • Kutangaza Injili ili watu wamwamini Kristo kama Bwana. • Kuanzisha makanisa ambamo watu watafuaswa na kuzaa matunda. • Kusaidia Kanisa kuishi dhamira yake ya kuleta uhuru, ustawi na haki ulimwenguni. Hivyo: Theolojia inayozingatia vyema Ufalme. . . kamwe haiwezi kupuuza kutoa wito wa wokovu kwa watu wa jamii zote na jumuiya za kidini. Kwa kila mtu wa imani yoyote ya kidini ujumbe huu lazima urudiwe: “Ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.” ... Theolojia yenye msingi wa Ufalme inahusisha wito wa kutambua ubwana wa Mfalme na mwelekeo mpya wa utii kwa katiba ya Ufalme wake. Kipengele hiki kisipokuwepo, haiwezekani kutangaza habari njema za Injili. Theolojia na misiolojia inayoongozwa na uelewa wa kibiblia wa utawala wa Kristo haitakosa kamwe kutambua wokovu wa mtu binafsi kama mojawapo ya malengo yanayojumuishwa katika Ufalme wa Mungu . . . Kanisa. . . linainuliwa na Mungu katika mataifa yote ili kushiriki katika wokovu na utumishi wenye mateso wa Ufalme. . . Kanisa ndilo mzaliwa wa kwanza, malimbuko ya Ufalme. Kwa hiyo, ingawa Ufalme sio tu kwa ajili ya Kanisa, Ufalme haufikiriki pasipo Kanisa. Kinyume chake, ukuaji na upanuzi wa Kanisa haupaswi kuangaliwa kama makusudi bali kama njia ya kutumika katika huduma ya Ufalme. . . . Funguo za Ufalme zimetolewa kwa Kanisa. Halitimizi agizo lake kwa kuachia funguo hizo bali kwa kuzitumia kufungua njia za kuufikia Ufalme kwa watu wote na makundi yote ya watu katika kila ngazi ya jamii za wanadamu. . . Mwisho, Injili ya Ufalme inajielekeza kwenye mahitaji yote muhimu ya kibinadamu, ya kimwili na kiakili. Inalenga kurekebisha kile ambacho kimeharibika katika dunia. Inalazimu kujihusisha katika mapambano ya haki za rangi, kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa.... Habari njema ya Ufalme inahusiana na mambo hayo yote. Kwa

Made with FlippingBook Digital Publishing Software