Theolojia Katika Picha
/ 2 0 9
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maandiko kuhusu Ufalme katika Agano Jipya
Mathayo 3:2 - Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Mathayo 4:17 - Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 4:23 - Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Mathayo 5:10 - Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Mathayo 5:19-20 - Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mathayo 6:33 - Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Mathayo 7:21 - Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 8:11-12 - Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Mathayo 9:35 - Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Mathayo 5:3 - Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Mathayo 6:10 - Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software