Theolojia Katika Picha
2 1 0 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maandiko kuhusu Ufalme katika Agano Jipya (muendelezo)
Mathayo 10:7 - Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 11:11-12 - Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Mathayo 12:25-26 - Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? Mathayo 12:28 - Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Mathayo 13:11 - Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. Mathayo 13:19 - Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. Mathayo 13:24 - Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake. Mathayo 13:31 - Akawatoleamfanomwingine, akisema, Ufalme wambinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake. Mathayo 13:33 - Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia. Mathayo 13:38 - lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu. Mathayo 13:41 - Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software