Theolojia Katika Picha
/ 2 3 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
4. Kwamba hata wale ambao hawajaokoka na walio katika uasi dhidi ya Mungu wategemee uumbaji wake na karama za neema (japokuwa zimekandamizwa, zikupotoshwa, au kuelekezwa katika njia ya uovu) kwa ajili ya uhai wao na kuwa na tija.
a. 1 Wakorintho 4:7 – Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? (Linganisha na Zab. 104.)
b. Mathayo 5:45- …ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
c. “Mungu yeye yule ndiye Mungu wa uumbaji na wa uumbaji mpya, atendeaye kazi hayo yote mawili kwa mapenzi yake makamilifu…. Kusudi lenye neema la Mungu kwa kila mmoja wetu ni la milele. liliundwa na hata “kutolewa” kwetu katika Kristo “kabla ya wakati wa milele” (2 Tim. 1:9, kama lilivyo); Mungu alituchagua tuwe watakatifu na akatuweka kuwa wana wake kupitia Yesu Kristo “kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Efe. 1:4,5); na kazi njema ambazo kwa ajili yake ziliumbwa upya katika Kristo ni zile hasa “ambazo Mungu alizitayarisha tangu mwanzo.” Ukweli huu wa msingi kwamba Mungu alipanga mwisho tangu mwanzo unapaswa kutuonya dhidi ya … [kutenganisha kwa urahisi sana] … kati ya asili na neema, kati ya maisha yetu kabla ya kuokoka na maisha yetu ya baada ya kuokoka” (John R. W. Stott, Baptism and Fullness: The Work of the Holy Spirit Today). B. Mtazamo wa 2 – Karama za rohoni ni uwezo mpya usio wa kawaida unaotolewa kwa Wakristo ambao unapatikana kwetu tu kupitia nguvu za Mungu na unaweza kutimiza mambo yaliyo mbali sana na uwezo wa mwanadamu. Mtazamo huu unakusudiwa kulinda ukweli kwamba:
1. Wokovu unaweza kubadilisha na kurejesha.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software