Theolojia Katika Picha

2 3 2 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)

2. Mungu anaweza kutoa chochote kinachohitajika katika mazingira fulani bila kujali rasilimali tunazoonekana kuwa nazo. Tunategemea Roho wa Mungu, si rasilimali zetu wenyewe.

3. Nguvu zisizo za kawaida zinazozidi chochote kinachowezekana katika uumbaji wa asili zinapatikana katika mwili wa Kristo.

4. Sisi sote tumeagizwa kutafuta karama fulani za rohoni ambazo zina manufaa kwa mwili (1 Kor. 12:31 & 14:12). Karama daima hutajwa kwa kurejelea jinsi zinavyotumika kuujenga mwili wa Kristo. Hakuna mahali katika Maandiko ambapo karama za rohoni zinatajwa nje na matumizi yake katika utendaji kazi ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa. a. 1 Wakorintho 1:26-29 – Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. b. Wasio Wakristo wana vipaji kupitia neema ya kawaida ( common grace )… lakini hivi ni vipaji, sio karama. Hakuna asiyeamini aliye na karama ya rohoni. Waamini pekee ndio wamejaliwa karama za rohoni…. Vipaji vinategemea nguvu za asili, karama hutegemea uwezesho wa kiroho. (Leslie B. Flynn, 19 Gifts of the Spirit).

C. Mtazamo wa 3 – Mtazamo wa kati ambao unaonyesha kwamba karama za rohoni zinaweza kuwa ama kuhuishwa na kutiwa nguvu kwa vipaji vya asili vilivyotolewa na Mungu au kuumbwa kwa vipaji vipya kabisa.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software