Theolojia Katika Picha
/ 2 3 3
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
1. Kumbuka kwamba kimantiki, angalau, si lazima kwa maoni haya mawili kukinzana. Angalau inawezekana kwamba aina zote mbili za karama za kiroho zipo, zingine ambazo zimefichwa na zingine ni mpya.
2. Pengine njia yenye manufaa zaidi ya kufikiria kuhusu hili itakuwa kukumbuka kwamba karama ni “udhihirisho” wa Roho kwa manufaa ya wote.
3. Mkazo zaidi hapa ni kudhihirishwa kwa Roho na si namna ambayo udhihirisho huo unatokea. Hili linapotokea daima huwa ni “kipawa cha neema”. Mara zote hutokea kwa sababu tu ya uamuzi wa Roho na kwa sababu ya nguvu zake. Kwa hivyo, ikiwa Roho atachagua kuwezesha uwezo wa asili au kuunda mpya kabisa, kila moja ni “ charisma ” – kipawa cha neema. Uwezo wa kufundisha unaotumiwa na mtu asiye mwamini alipewa na Mungu na ni kipawa cha neema (iliyotolewa na Roho katika uumbaji), lakini sio “udhihirisho wa Roho” hadi mtu huyo ajinyenyekeze kwa Roho Mtakatifu na kutumia karama hiyo chini ya maelekezo na kwa makusudi yake.
II. JeKaramaZoteZilizoorodheshwakatikaAgano Jipya zinapatikana leo?
A. Baadhi ya mapokeo (imani za madhehebu) hujibu “Hapana.”
1. Baadhi ya mapokeo yanabishana kuhusu kukoma kwa karama fulani: kwa kawaida utume, unabii, lugha na tafsiri (wakati fulani miujiza).
2. Kuna angalau sababu mbili za kitheolojia kwa nini hii inaaminika hivyo.
a. Kwanza, kuna wasiwasi wa kulinda ufunuo wa Mungu katika Maandiko.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software