Theolojia Katika Picha
2 3 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
Ikiwa mitume, manabii, na lugha vitaendelea kufanya kazi kama njia ya ufunuo unaoendelea, uadilifu wa Maandiko unaweza kuwekwa hatarini. Tena na tena katika historia ya Kanisa, watu wametokea ambao walidai wamepata ufunuo mpya wa kinabii ambao ulipingana na Maandiko au hata kwenda nje sana ya mafundisho yake. Ushuhuda wa kimaandiko juu ya Yesu kama Neno la mwisho la Mungu haupaswi kupotoshwa, na mapokeo haya ya kitheolojia hayaoni njia ya kupatanisha uwezekano wa mafunuo mapya na ukweli huo. b. Pili, jukumu la mitume kama “msingi” wa Kanisa linaonekana kuashiria nafasi ya kipekee katika historia ya Kanisa. Vitabu vya injili na Kitabu cha Matendo ya Mitume vinaonekana kama msingi wa historia ambapo Mungu anafanya kazi ya kipekee na bila kurudia kubadilisha ufunuo wake kutoka kwa Agano la Kale hadi Agano Jipya. Hili linatimizwa kwa kutoa mafunuo mapya (ambayo yanaunda Maandiko ya Agano Jipya) na ishara na maajabu ambayo yanathibitisha na kuwekea msingi ushuhuda huu kuwa wa kweli. Kanisa sasa linapaswa kuishi kwa ushuhuda wa Neno hilo, likilinda amana ya imani lakini sio kuiongeza au kuipunguza. 1) Yuda 1:3 – Wapenzi, ijapokuwa nilitaka sana kuwaandikia juu ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. (2) Waebrania 1:1-3 – Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu; (3) Wagalatia 1:8-9 – Lakini hata ikiwa sisi au malaika kutoka mbinguni atawahubiri ninyi injili tofauti na ile tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, Mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili kinyume na ile mliyoipokea, na alaaniwe.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software