Theolojia Katika Picha
/ 2 3 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
B. Baadhi ya mapokeo (imani za madhehebu) hujibu “Ndiyo.” “Wote wanaweza kukubaliana kwamba hakuna ufunuo mpya unaoweza kutarajiwa kuhusu Mungu katika Kristo. Lakini inaonekana hakuna sababu nzuri kwa nini Mungu aliye hai, ambaye hunena na kutenda (tofauti na sanamu zilizokufa), hawezi kutumia karama ya unabii kutoa mwongozo kwa kanisa la mahali fulani, taifa au mtu binafsi, au kuonya au kutia moyo kwa njia ya kutabiri na kwa maonyo, sawasawa na neno lililoandikwa la Maandiko Matakatifu, ambalo kwa hilo maneno hayo yote lazima yajaribiwe. Ni kweli, Agano Jipya halionyeshi kuwa kazi ya nabii ni kuwa mvumbuzi wa mafundisho, bali kutoa neno ambalo Roho humpa kulingana na kweli waliokabidhiwa mara moja watakatifu (Yuda 3), kuchochea na kutia moyo imani yetu.” (J. P. Baker, “Prophecy,” New Bible Dictionary, 2 nd Edition, J. D. Douglas and Others, eds).
1. Huduma ya Yesu na mfano wa Mitume na Kanisa la Agano Jipya ni kielelezo chetu kilichovuviwa kwa ajili ya huduma na wote walitumia karama za miujiza katika huduma.
2. Wakati pekee ambapo Maandiko yanazungumzia swali la lini karama zitakoma yanarejelea kurudi kwa Kristo (1 Kor. 13:8-12).
3. Roho Mtakatifu ana uhuru na ni mwenye enzi. Anaweza kutoa (au kutokutoa) karama yoyote wakati wowote kwa kusudi lolote kama apendavyo ( 1 Kor. 12:11 – anatoa atakavyo yeye).
4. Andiko la Craig S. Keener (Gift and Giver— kurasa za 89-112 ) linatoa hoja za msingi kwa mtazamo huo kwamba zote zinapatikana.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software