Theolojia Katika Picha
2 4 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Mambo ya Jumla Kuhusu Agano Jipya (muendelezo)
Mambo ya Jumla kuhusu Agano Jipya
1. A gano Jipya ni agano la kazi ya Mungu ya kuokoa katika zama hizi na linamtangaza Mwokozi ambaye Agano la Kale lilimngojea. 2. A gano Jipya lina vitabu 27, vinne viitwavyo Injili vinavyohusu maisha na huduma ya Yesu, kimoja kinahusu historia ya Kanisa, yaani Matendo ya Mitume , na Nyaraka au barua 21, na kitabu kimoja cha unabii . 3. M kusanyiko wa vitabu katika Agano Jipya unajumuisha kanuni , yaani mkusanyo ulioidhinishwa ambao ulikusanywa kwa zaidi ya karne 3. 4. H ati za AJ ziliandikwa kwanza kwenye mafunjo (karatasi iliyotengenezwa kwa matete, na kisha kwenye ngozi). Takriban nyingine 300 zimeandikwa kwa herufi kubwa ( uncials ), kwa kawaida kwenye ngozi. Kundi kubwa zaidi ni lile la herufi ndogo ( minuscules ) na zinakuwa katika aina ya maandishi yaliyoviringwa na kuunganishwa ambayo yalivumbuliwa huko Byzantium takriban karne ya tisa. Vitabu vya ibada , vinavyotumika katika ibada ya Kanisa, vinajumuisha sehemu za Maandiko pia. 5. A gano Jipya linaaminika kwa sababu ya 1) ushahidi mwingi unaoliunga mkono; 2) waandishi waliandika ndani ya kizazi cha kwanza au cha pili cha historia ya Kikristo, na 3) matoleo ya kale yalisambazwa sana. 6. T oni ya kibinafsi ya Agano Jipya inaonekana katika ukweli kwamba kati ya vitabu 27, 24 ni barua binafsi, na 3 ni simulizi binafsi za maisha na kazi ya Kristo. 7. A pokrifa inajumuisha vitabu 14 visivyo vya kikanuni vilivyoandikwa kati ya 200 K.K na 100 B.K. 8. W ayahudi walimwona Yesu kuwa tishio kwa sababu waliamini alitoa madai yenye utata kwa habari yake mwenyewe na kuchukulia desturi za Kiyahudi kwa wepesi. 9. Y esu alitokea wakati ambapo mapokeo ya Dini ya Kiyahudi yaliongoza maisha na desturi nyingi za Kiyahudi. Ufahamu wa desturi hizi unaweza kusaidia sana uelewa wetu wa Agano Jipya.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software