Theolojia Katika Picha

2 5 2 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Maono ya Kinabii kama Chanzo cha Kuikubali Imani ya Kibiblia Mch. Dkt. Don L. Davis

Imani ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu. Wanadamu ni viumbe vya kukiri, kuamini na kutegemea. Na mahali tunapoweka imani yetu huamua mtazamo wa ulimwengu tutakaouchukua. Kwa maneno mengine, maamuzi yetu ya mwisho ya aina ya imani tunayoikubali ndiyo huweka mipaka ya mtazamo wetu wa ulimwengu. Imani inachonga maono yetu kuhusu mfumo wa maisha. Watu wanaotilia shaka mtazamo wao wa ulimwengu hawana utulivu na wanahisi hawana msingi wa kusimamia. Mara nyingi wanakuwa katika hali ya shida ya kisaikolojia. Lakini mzozo wa kihisia kimsingi ni wa kidini kwa sababu mtazamo wetu wa ulimwengu unategemea imani kunayoamua kuikubali. Kuikubali imani maana yake nini? Ni namna tunavyojibu maswali manne ya msingi yanayomkabili kila mtu: 1) Mimi ni nani? Au, asili, kazi, na kusudi la wanadamu ni nini? 2) Niko wapi? Au, nini hali na asili ya dunia na ulimwengu ninamoishi? 3) Tatizo ni nini? Au, ni tatizo gani la msingi au kizuizi kinachonizuia kufikia ukamilifu na ustawi? Kwa maneno mengine, ninauelewaje uovu? 4) Dawa ni nini? Au, inawezekanaje kushinda kizuizi hiki cha ukamilifu na ustawi wangu? Kwa maneno mengine, ninawezaje kuupata wokovu? Tunapojibu maswali haya, yaani, imani yetu inapotulia, ndipo tunaanza kuona uhalisia wa mambo katika taswira fulani yenye busara na ya kueleweka. Kutokana na imani yetu huja mtazamo wa ulimwengu, ambao bila huo maisha ya mwanadamu hayawezi kuendelea. ~ Brian J. Walsh and J. Richard Middleton. The Transforming Vision . Downers Grove: InterVarsity Press, 1984. uk. 35.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software