Theolojia Katika Picha

/ 2 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Dhana za Ufalme Howard A Snyder, Machi 2002.

1. Ufalme kama Tumaini la Wakati Ujao – Ufalme Ujao

Hii imekuwa dhana kuu katika historia ya Kanisa. Msisitizo mkubwa ni juu ya siku zijazo: kilele cha mwisho na upatanisho wa vitu vyote, jambo ambalo ni zaidi ya hali ya roho kuishi katika umilele. Dhana hii imejengwa zaidi kwenye maandiko ya Agano Jipya. Ingawa baadhi dhana zifuatazo pia zinawakilisha tumaini la siku zijazo, hapa dokezo la maisha yajayo limewekewa mkazo mkubwa zaidi.

2. Ufalme kama Hali ya Ndani ya Kiroho – Ufalme wa Ndani

“Ufalme wa kiroho” ambao mtu anaupokea katika moyo au nafsi; “maono mazuri.” Dhana ya kifumbo sana, na kwa sababu hiyo ni ya kibinafsi; uzoefu ambao huwezi kushirikisha wengine. Mifano: Julian wa Norwich, watawa wengine; pia baadhi ya mifano ya Kiprotestanti ya kisasa.

3. Ufalme kama Ushirika wa Kifumbo – Ufalme wa Mbinguni

“Ushirika wa watakatifu”; Ufalme ambao kimsingi unahusishwa na mbingu. Ubinafsi mdogo. Mara nyingi hujikita hasa katika ibada na liturujia. Mifano: Yohana wa Damasko, John Tauler; kwa namna fulani tofauti, Wesley na uamsho na Uprotestanti wa Kiinjili wa karne ya 19 na 20. Ufalme kimsingi ni wa ulimwengu mwingine na wa siku zijazo.

4. Ufalme kama Kanisa la Kitaasisi – Ufalme wa Kikanisa

Mtazamo mkuu wa Ukristo wa zama za kati; ulitawala katika Ukatoliki wa Kirumi hadi Vatikani ya II. Papa kama Kasisi wa Kristo anatawala duniani badala ya Kristo. Mvutano kati ya Kanisa na Ufalme kwa kiasi kikubwa unaisha. Chimbuko lake ni katika dhana ya “Mji wa Mungu” ya Augustine, lakini iliendelezwa tofauti na kile ambacho Augustine aliamini. Tofauti za Kiprotestanti huonekana wakati wowote Kanisa na Ufalme vinapofungamana kwa ukaribu sana. Mawazo ya kisasa ya “Ukuaji wa Kanisa” yamekosolewa katika hatua hii.

5. Ufalme kama Mfumo Kinzani – Ufalme wa Kimapinduzi

Huenda dhana hii iliibuka kama matokeo ya kuipinga dhana namba 4; yenyewe huona Ufalme kama mfumo halisi ambao una jukumu la kinabii la kuhukumu

Made with FlippingBook Digital Publishing Software