Theolojia Katika Picha

2 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Dhana za Ufalme (muendelezo)

mfumo wa kijamii na wa kisiasa kadhalika na Kanisa. Moja ya mifano bora: Fransisko wa Assisi; pia Wana-Mageuzi Wenye Itikadi Kali wa karne ya 16; “Wakristo wenye msimamo mkali” wa leo; Jarida la Sojourners . Dhana hii Hulichukulia Kanisa kama mfumo kinzani dhidi ya mila na tamaduni na ambao unaakisi utaratibu mpya wa Ufalme.

6. Ufalme kama Dola ya Kisiasa – Ufalme wa Kitheokrasia

Ufalme unaonekana kama theokrasia ya kisiasa; Kanisa na jamii si lazima viwe katika mfumo wa kidemokrasia. Huelekea kujenga misingi yake katika vielelezo vya Agano la Kale, hasa Ufalme wa Daudi. Mfano wa Konstantini; Ukristo wa Bizantini ni mfano mzuri. Geneva ya Calvin, pengine, kwa maana tofauti. Tatizo la dhana ya “falme mbili” ya Luther.

7. Ufalme kama Jamii ya Wakristo – Ufalme Unaoleta Mabadiliko

Hapa pia Ufalme unatoa kielelezo kwa jamii, lakini zaidi katika suala la maadili na kanuni zinazopaswa kutekelezwa katika jamii. Ufalme katika utimilifu wake ungekuwa jamii inayotawaliwa kikamilifu na maadili ya Kikristo. Baada ya milenia; Wainjilisti wengi wa katikati ya karne ya 19; Injili ya Kijamii ya mwanzoni mwa karne ya 20. Ufalme unadhihirika hatua kwa hatua katika jamii, tofauti na imani ya kabla ya milenia. 8. Ufalme kama Jamii Kamilifu ya Kufikirika ya Kidunia – Ufalme wa Kidunia Dhana hii inaweza kuonekana kama dhana namba 7 iliyozingatiwa kupita kiasi (au ‘kutiwa chumvi’). Dhana hii ya Ufalme kiuhalisia ni ya kufikirika tu. Huelekea kukataa au kudharau dhambi, au kuona uovu kama mazingira tu. Mtazamo wa jamii nyingi za kufikirika (Cohn, Pursuit of the Millennium ) ukijumuisha mifano ya Marekani na Uingereza za karne ya 19. Kwa njia tofauti, maoni ya wengi wa Mababa Waanzilishi wa Marekani. Mfano wenye ushawishi mkubwa wa karne ya 20: Umaksi. Theolojia ya Ukombozi, kwa kiwango fulani. Kwa njia tofauti kabisa: Utawala wa Milenia wa Marekani, ukichanganya dhana hii na namba 1, 2 na/au 3 – Ufalme hauna umuhimu wa kisasa, lakini utakuwa jamii kamilifu (ya kufikirika) halisi katika siku zijazo. Hivyo kuna kufanana kati ya Umaksi na Ufandamentalisti.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software