Theolojia Katika Picha

2 9 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Mifumo ya Upandaji Makanisa Mch. Dkt. Don L. Davis

Maswali yafuatayo yameandaliwa ili kutusaidia kuangazia chaguzi mbalimbali zinazopatikana kwa wapanda makanisa wa mijini wenye tamaduni mbalimbali katika kuanzisha makanisa miongoni mwa watu maskini. Ni matumaini yetu kwamba mazungumzo yetu ya leo yatachambua baadhi ya masuala muhimu ambayo ni ya lazima kwa timu ya upandaji makanisa kutafakari ili kufanya maamuzi yake kuhusiana na aina ya kanisa wanalopaswa kupanda, kwa kuzingatia utamaduni, idadi ya watu, na mambo mengine wanayokumbana nayo katika uwanja wao mahususi wa utume.

1. Toa ufafanuzi wa kirai “mifumo ya upandaji makanisa.” Kwa nini inaweza kuwa muhimu kuzingatia chaguzi mbalimbali katika upandaji makanisa miongoni mwa watu maskini mjini?

2. J e, unawezaje kubainisha mifano mbalimbali (au mingine) ambayo inapatikana kwa timu ya wapanda makanisa wa mjini? Ni mambo gani unayoweza kufikiria kuwa ni nguvu za kila mfano na/au udhaifu wake kuhusiana na upandaji makanisa miongoni mwa watu maskini mjini? a. Mfumo wa mchungaji mwanzilishi – kiongozi anahamia katika jamii fulani kwa nia ya kuongoza na kuchunga kanisa ambalo amelipanda. b. Mfumo wa mgawanyiko wa kanisa?! – kanisa jipya linaundwa kwa sababu ya kutokubaliana kwa msingi juu ya suala fulani la maadili, tafsiri ya Biblia, au kutokana na mafarakano. c. Mfumo wa ukoloni – kusanyiko kubwa linatuma kundi zima (kwa kawaida likiwa na uongozi na washirika walioandaliwa tayari) katika jamii ambayo haijafikiwa kama aina ya kiini cha kanisa ambalo linakusudiwa kuanzishwa. d. Mfumo wa Kanisa Mama ( Beachhead Model ) – kusanyiko kuu, imara linaamua kuwa aina fulani ya kituo cha kutuma na makao makuu ya malezi ya makanisa mapya yaliyopandwa kupitia uangalizi na ufadhili wake, katika eneo la karibu na/au la mbali na mipaka yake. e. Mfumo wa Kanisa Seli ( Cell Church ) – kusanyiko lililowahi kuwa kuu ambalo msingi wa maisha na huduma yake uko katika seli ambazo zimeunganishwa kimuundo na kichungaji na kusanyiko kuu; ushiriki wao pamoja ndio unaounda kanisa.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software