Theolojia Katika Picha

/ 3 0 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Mtazamo wa Kristo Kuhusu Biblia Paul P. Enns. The Moody Handbook of Theology (Electronic Ed.). Chicago: Moody Press, 1997.

Katika kutambua asili ya uvuvio wa Biblia, hakuna ambacho kinaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana zaidi ya kutambua mtazamo wa Kristo uliopo kuhusiana na Maandiko. Hakika hakuna yeyote anayeruhusiwa kuyatazama Maandiko kwa mtazamo wowote wa chini zaidi ya ule ambao Yesu alikuwa nao; mtazamo wake wa Maandiko ndio unatakiwa kuwa mtazamo wa kielelezo na desturi kwa mitazamo ya watu wengine. Hiyo ndio hoja kuu ya Mwanathiolohia, Profesa R. Laird Harris. Katika kutetea uvuvio wa Maandiko hatumii Maandiko ya 2 Timotheo 3.16 au 2 Petro 1.21 kama Maandiko ya msingi kwa hoja hiyo, (ingawa anatambua uhalali wake); badala yake anatetea hoja kutoka msingi wa mtazamo wa Kristo wa Maandiko. (1) Kuvuviwa kwa kitabu chote. Katika kutumia kwake Agano la Kale Kristo alitoa uthibitisho kwa uvuvio wa Agano la Kale lote. Katika Mathayo 5.17–18 Kristo anathibitisha kwamba hakuna hata nukta wala yodi ambayo itaondolewa kutoka kwenye torati hata yote yatimie . Katika msitari wa. 17 alilenga kwenye sheria au manabii, kauli ya kawaida inayoelezea Agano lote la Kale. Katika kauli hii yenye nguvu, Yesu alithibitisha kutokuwa na makosa kwa Agano zima la Kale na hivyo akathibitisha uvuvio wa Agano zima la Kale. K atika Luka 24.44 Yesu anawakumbusha wanafunzi wake kwamba vitu vyote vilivyoandikwa kuhusu yeye katika torati ya Musa, manabii, na Zaburi lazima vitimie. Wanafunzi walishindwa kuelewa mafundisho kuhusiana na kifo na kufufuka kwa Kristo katika Agano la Kale, lakini kwa sababu ya kuvuviwa kwa Agano la Kale, yale matukio yaliyo tabiriwa yalitakiwa kutokea. Kwa kutoa kwake sifa za Agano la Kale, Kristo alikuwa anathibitisha kuvuviwa kwa mamlaka ya Agano zima la Kale. Y esu alipokuwa akishindana kwa hoja na Wayahudi wasioamini kuhusiana na haki yake kuitwa Mwana wa Mungu, aliwapeleka kwenye Zaburi 82.6 na kuwakumbusha “Maandiko hayawezi kutanguka” (Yohana 10.35). “ina maana kwamba Maandiko hayawezi kuondolewa nguvu yake kwa kuonyeshwa kwamba” Ni lazima izingatiwe kwamba Yesu alinukuu hata Maandiko kutoka kwenye Agano la Kale ambayo kwa haraka yanaonekana kama hayana uzito sana na hivyo kuonyesha kwamba Maandiko hayawezi kutenganishwa au kubatilishwa. (2) K uvuviwa kwa sehemu tu za Maandiko. Kristo alinukuu mara nyingi kutoka kwenye Agano la Kale. Hoja zake zilijikita zaidi katika uaminifu Maandiko ya Agano la Kale aliyokuwa ana nukuu. Njia hii ya mijadala inapendekeza kwamba, Kristo alikuwa anathibitisha uvuvio wa sehemu moja moja au vitabu vya Agano la Kale. Mifano michache itatosha. Yesu alipokutana na Shetani katika kipindi cha jaribu lake.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software