Theolojia Katika Picha
3 0 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Mtazamo wa Kristo Kuhusu Biblia (muendelezo)
Aliyashinda majaribu ya Shetani kwa kutumia kitabu cha Kumbukumbu la Torati katika Mathayo 4.4, 7, 10 Yesu ananukuu kutoka kitabu cha Kumbukumbu la Torati 8.3; 6.13, 16, akionyesha kwamba Shetani hakuwa sahihi na kusisitiza kwamba maneno haya yaliyoandikwa katika Kumbukumbu la Torati yalitakiwa kutimia. Katika Mathayo 21.42 Yesu alinukuu kutoka Zaburi 118.22, ambayo inafundisha kwamba Masihi atakataliwa. Katika Mathayo 12.18–21 Yesu alinukuu kutoka Isaya 42.1–4, akionyesha kwamba kufanya kwake amani, hali ya upole na ujumuishaji wa mataifa, yote yalishakuwa yametabiriwa zamani katika maandishi ya kinabii. Hii ni mifano tu michache tuliyoichagua, inayofunua kwamba Kristo alinukuu sehemu mbalimbali za Agano la Kale, akithibitisha uvuvio wake na mamlaka. (3) K uvuviwa kwa maneno. Katika kutetea fundisho la kiyama kwa Masadukayo, Yesu ananukuu kutoka kitabu cha Kutoka 3.6 (ni muhimu kwasababu Masadukayo walikuwa wanavishikilia vitabu vitano tu vya Musa), “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu.” Katika majibu haya, majibizano yote ya Yesu alijikita kwenye maneno “Mimi Niko.” Yesu alikuwa anasambaza maneno hayo ambayo yalikuwa na yana maana sana kwa Maandiko ya kiebrania tu. Na hivyo alikuwa anaunga mkono Septuajinti (toleo la kiyunani la Biblia yaKiebrania) toleo lililohusishamaneno hayo. Toleo hilo lilichukuliwa na wengi waliokuwepo nyakati za Bwana Yesu kwamba lilikuwa linawekwa kiwango sawa na Maandiko ya asili. K atika kuthibitisha ufufuo, Yesu aliwakumbusha Masadukayo, kwamba Kut 3.6 akasema “Mimi niko.” Akaelezea: “Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai” Kama maneno ya Agano la Kale hayakuwa yamevuviwa, basi hoja zake zilikuwa ni bure; lakini kama maneno yale yalikuwa yamevuviwa basi hoja zake zinabeba uzito mkubwa. Kwakweli, mjadala wa Yesu unajikita kwenye wakati uliopo wa kauli ile. Kwa sababu iliandikwa kwenye kitabu cha Kutoka 3.6 “Mimi niko.…” , fundisho la ufufuo linaweza kuthibitishwa; Mungu ni Mungu wa mababa wa imani walio hai. M fano kama huo unapatika katika Mathayo 22.44 ambapo Yesu anabishana na mafarisayokwambamtazamowao juudhana yaMasihi ilikuwa siosahihi.Mafarisayyo walimfikiria Masihi kama mkombozi wa kisiasa lakini Yesu anawaonyesha kutoka kwenye nukuu yake katika Zaburi 110.1 kwamba Daudi, Mfalme mkuu zaidi wa Israeli alimuona Masihi kama mkuu zaidi yake yeye, hata akamwita Bwana. Mdahalo wote wa Kristo unaelezea kuhusu neno “Bwana wangu” Katika kunukuu Zaburi 110.1 Yesu aliweka hoja yake katika uvuvio wa maneno mafupi “Bwana wangu” Kama Zaburi 110.1 haikuwa inasomeka “Bwana wangu” Basi hoja zote za Yesu zilikuwa hazina nguvu. Mfano wa nyongeza ni Kristo kutumia Zaburi 82.6 katika Yohana 10.34 ambapo hoja zake zote zinalenga katika neno “miungu”
Made with FlippingBook Digital Publishing Software