Theolojia Katika Picha

/ 3 1 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)

3. “Wakati wote [katika historia ya Kanisa] hakujakosekana watu wenye roho ya unabii, kwa kweli si kwa ajili ya kutangaza fundisho lolote jipya la imani, bali kwa ajili ya mwelekeo wa matendo ya kibinadamu” (Thomas Aquinas, Summa Theologica , Buku la 5, Westminster, MD: Christian Classics, © Benziger Brothers, 1948, uk. 1906). 4. “[Unabii] ulipewa mamlaka isiyo na shaka baada tu ya kuhakikiwa (rej. 1 The.5:19-21). Hata ulipotambuliwa kuwa neno la kimungu, haikuwa lazima liwe neno la kikanuni. Unabii ulikuwa na (na una) matumizi muhimu kwa wapokeaji wake wa karibu lakini ulipewa hadhi ya kikanuni tu wakati ulipotambuliwa pia kuwa ufunuo wa kikanuni kwa vizazi vijavyo na kipimo ambacho kwacho unabii ujao unaweza kujaribiwa” (E. E. Ellis, “Prophecy, Theology of ” New Dictionary of Theology, Sinclair Ferguson, David F. Wright, na J. I. Packer, wahariri, Downers Grove, IL/Leicester, England: InterVarsity Press, 1988, uk. 538). 5. Wayne Gruden anatoa hoja katika kitabu chake The Gift of Prophecy in the New Testament and Today , (Wheaton, IL: Crossway Books, 2000) kwamba manabii wa Agano la Kale na Mitume wa Agano Jipya (kwa maana finyu ya wale Kumi na Wawili pamoja na Paulo) kiutendaji wanafanana kwa kuwa wao ndio watu pekee walioidhinishwa kutoa ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu ambao hauwezi kubatilishwa. Kilicho kweli kwa manabii wa Agano la Kale pia ni kweli kwa mitume wa Agano Jipya kwa kuwa wote hawa wanazungumza kwa mamlaka ambayo yanazidi yale ya manabii wa Agano Jipya. Kwa maneno mengine, nabii wa Agano Jipya hasemi kwa niaba ya Mungu kwa namna sawa na nabii wa Agano la Kale au mtume wa Agano Jipya (kwa maana ile finyu). Mtazamo huu unaungwa mkono na D.A. Carson ambaye anaandika hivi: “Ni hoja yenye nguvu kwamba mfano wa kweli wa Agano Jipya wa nabii wa Agano la Kale sio nabii wa Agano Jipya bali ni mtume wa Agano Jipya (kwa maana finyu).... Kwa hakika haiwezekani kufikiria 1 Kor. 14:29 ikitumika kwa manabii wa Agano la Kale (mara sifa zao zilipothibitishwa) au kwa mitume wa Agano Jipya. ( Ona “Church, Authority in,” The Evangelical Dictionary of Theology , Walter A. Elwell, mhariri, Grand Rapids: Baker Book House, 1984, uk. 228-229.)

Made with FlippingBook Digital Publishing Software