Theolojia Katika Picha
3 1 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
lingeweza pia kutumiwa kuelezea manabii wasio rasmi sana kama vile wale wanaojihusisha na ubashiri wa kinabii, na washairi ambao walitunga chini ya ushawishi wa utendaji wao. Unabii mwingi katika ulimwengu wa Wayunani ulikuwa wa uaguzi ambapo mtu alimwendea nabii na kuuliza swali ambalo nabii huyo alilijibu. Katika mawazo ya Kiyunani, “Nabii anachukua nafasi ya upatanishi. Yeye ndiye msemaji wa mungu na pia ni msemaji wa mwanadamu kwa mungu huyo.” ( Kamusi ya Kitheolojia ya Agano Jipya , Buku la 6 , Gerhard Kittel, mhariri, Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans, 1964, uk. 794). B. Nukuu Husika za Kitheolojia 1. “Sote tunaweza kukubaliana kwamba hakuna ufunuo mpya unaoweza kutarajiwa kuhusu Mungu katika Kristo. Lakini inaonekana hakuna sababu nzuri kwa nini Mungu aliye hai, ambaye hunena na kutenda (tofauti na sanamu zilizokufa), hawezi kutumia karama ya unabii kutoa mwongozo wa mahali fulani kwa kanisa, taifa au mtu binafsi, au kuonya au kutia moyo kwa njia ya kutabiri na kutoa kumbusho fulani, sawasawa na neno lililoandikwa la Maandiko, ambalo kwa hilo maneno hayo yote lazima yapimwe. Hakika Agano Jipya halioni kama kazi ya nabii ni kuwa mvumbuzi wa mafundisho, bali kutoa neno ambalo Roho amempa kulingana na kweli waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu (Yuda 3), kutoa changamoto na kutia moyo imani yetu” (J. P. Baker, “Prophecy,” New Bible Dictionary , Toleo la 2, J. D. Douglas na wengine, mhariri, Leicester, England-Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1982, uk. 985). 2. “Nabii anajua kitu fulani cha siri za kiungu.... Lakini, unabii wa Kikristo wa zamani haujumuishi tu ufunuo wa matukio yajayo.... Nabii anazungumza juu ya masuala ya sasa. Hasemi tu kile ambacho Mungu anakusudia kufanya; pia anatangaza kile ambacho Mungu angefanya na wanadamu.... Nabii anawaonya wavivu na waliochoka na kuwafariji na kuwatia moyo wale wanaoshambuliwa, 1Kor. 14:3; Ac. 15:32. Kupitia mahubiri yake anafunua uovu wa siri wa wanadamu, 1Kor. 14:25. Kwa kuwa yeye husema kwa haiba ya mamlaka aliyopewa na Mungu, anatoa maagizo yenye mamlaka, ingawa yeye mwenyewe hayuko juu ya agizo la kibiblia kuhusu ukosoaji” ( Gerhard Kittel, mhariri, Theological Dictionary of the New Testament , Buku la 6, Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans , 1964, uk. 848).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software