Theolojia Katika Picha

/ 3 1 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)

ambayo mwandishi mwenyewe anaonekana kuwa nayo), linaonyesha kwamba kushindwa kwa waalimu kutaleta adhabu kali siku ya hukumu” ( K. Wegenast, The New International Dictionary of New Testament Theology, Buku la 3, Colin Brown, Mhariri Mkuu, Grand Rapids: Zondervan, 1986, uk. 768). C. Muhtasari Msingi wa ofisi ya ualimu ni uwezo wa kufafanua Maandiko kwa namna ambayo makusanyiko na watu binafsi ndani yake wanapokea “amana ya Imani,” na kupinga mafundisho ya uongo kwa njia ya kweli ya Maandiko. Kwa sababu wanalinda mafundisho yenye uzima, ni muhimu wale wanaoshikilia “ofisi” ya ualimu watambuliwe rasmi na wapewe mamlaka ya kusema kwa niaba ya kusanyiko. Wamishenari walio na karama za kufundisha lazima wafanye kazi kila mara ili kukabidhi mafundisho yenye uzima kwa “watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha wengine pia” (2 Tim. 2:2). A. Mazingatio ya Kiisimu Prophetes “Mtabiri” (“nabii”); kwa ulinganifu, mnenaji aliyevuviwa; katika maana ya ziada, mshairi ( Kamusi ya Kiyunani ya Strong ya Maneno ya Agano Jipya ) “‘Mtu anayesema wazi wazi,’ ‘mtangazaji wa ujumbe wa kiungu’. . . . Kwa ujumla, ‘nabii’ alikuwa mtu ambaye Roho wa Mungu alikuwa juu yake . . . mtu ambaye, kwake na kupitia kwake, Mungu alizungumza.” (W. E. Vine, Vine’s Complete Expository Dictionary of Old and New Testament Words , Nashville: Thomas Nelson, 1996, uk. 493). Katika utamaduni wa kale wa Kiyunani 2 , neno nabii lingeweza kutumika likimaanisha nabii wa uaguzi kama yule wa Delphi, ambapo lilitumika kwa uwazi kuelezea nafasi rasmi (ofisi). “Nabii mwaguzi anapata heshima ya kijamii kiasi kwamba anaweza kualikwa kutekeleza majukumu ya uwakilishi kama vile kuongoza wajumbe na kuwa msemaji wao. Sifa ya kiofisi ya cheo chake iko wazi kutokana na ukweli kwamba ilikuwa kawaida kuupa mwaka jina la kipindi chake cha uongozi” ( Kamusi ya Kitheolojia ya Agano Jipya , Buku la 6 , Gerhard Kittel, mhariri, Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans, 1964, uk. 792). Lakini,

2 Ingawa ni muhimu kuelewa muktadha wa lugha na wa kijamii wa ulimwengu wa Kiyunani ambao ni msingi wa neno ambalo Paulo analitumia hapa, labda kuna mwingiliano mdogo kati ya unabii unaojulikana katika ulimwengu wa Kiyunani na matumizi ya Paulo ya neno hilo ambayo ni ya Kiyahudi na ya Kikristo zaidi. Christopher Forbes anatoa hoja yenye nguvu kuhusu tofauti hizi katika kitabu chake cha Prophecy and Inspired Speech in Early Christianity and its Hellenistic Environment (Peabody: Hendrickson, 1997). Miongoni mwa mambo mengine, Forbes anaonyesha kwamba mifumo ya kijamii ambayo ilifafanua unabii wa Kikristo ilitofautiana sana na unabii wa Kiyunani. “Makundi ya Wakristo wa kwanza . . . hayakuwa na madaraja ya kikuhani, hakuna desturi za kinabii zilizorasimishwa kwa uangalifu zaidi ya kanuni chache rahisi za kiutaratibu . . . hakuna sehemu za kubashiria, na hakuna utaratibu uliohitajika wa namna ya kupata uaguzi. . . . unabii wa mwanzoni mwa Ukristo ulichukua sura tofauti kabisa na ile ya unabii katika ulimwengu mpana wa Uyunani” (uk. 319). Kinyume na unabii wa uaguzi wa utamaduni wa Kiyunani, “Unabii wa Kikristo wa awali ulikuwa wa kawaida katika angalau maana hii: mtu hakumwendea nabii na kuuliza jambo. Nabii alihutubia mkutano, bila kuuliza kabla, kwa ujasiri kwamba ufunuo wake ulikuwa neno la Mungu kwa hitaji lao, pasipo kujali kwamba hitaji hilo lilikuwa limefahamika kabla au la” (uk. 289).

IV. Manabii

Made with FlippingBook Digital Publishing Software