Theolojia Katika Picha
3 1 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
B. Nukuu Husika za Kitheolojia 1. “Maneno mchungaji na mwalimu yamewekwa pamoja kana kwamba hii ni ofisi moja, na kwa namna nyingi ndivyo ilivyo. Hata hivyo, kunaweza kuwa na waalimu ambao hawajaitwa kuwa wachungaji. Mwalimu ni yule anayefundisha, hasa katika fundisho la Biblia” ( Joe H. Cothen, Equipped for Good Work , Gretna, LA: Pelican Publishing, 1996, uk. 301). 2. “Maudhui ya fundisho hilo yalikuwa na upana mkubwa: yalijumuisha mafundisho ya Yesu pamoja na matokeo yake kwa imani na mwenendo wa Kikristo. Katika Matendo 2:42 linaitwa ‘fundisho la mitume,’ ambalo kanisa la kwanza la Yerusalemu linasemekana lilidumu katika hilo.... Katika kuiandikia Rumi, Paulo anafikiri kwamba ‘aina ya elimu’ ambayo Wakristo wa jiji hilo walikuwa wameipokea ilikuwa wazi vya kutosha na yenye kina kiasi cha kuwawezesha kutambua na kukataa propaganda ambayo haikupatana nayo (Rum. 6:17; 16:17 ).” (F. F. Bruce, “Waraka kwa Wakolosai, kwa Filemoni, na kwa Waefeso,” The New International Commentary on the New Testament , Buku la 10., Grand Rapids: Eerdmans, 1984, uk. 348-349). 3. “Tukumbuke kwamba Yesu hakuwa tu mchungaji , bali alikuwa mwalimu (kama tu alivyokuwa mtume , nabii na mwinjilisti ).... Mafundisho yake yalikuwa ni neno la Mungu lenye uzima. Mapema katika huduma yake, akijibu majaribu ya Shetani, Yesu alisema, “Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mt. 4:4).... Hivyo, kusudi kuu la mafundisho yote ya Kikristo ni kuwalisha watu Neno lile lile la uzima.... Kumbuka kwamba Petro aliamriwa na Yesu sio tu kuchunga kondoo wake—akimaanisha hasa kusimamia na kulinda— lakini pia kulisha wana-kondoo wake na kulisha kondoo wake. Kulisha huku kunaweza kutokea tu kupitia “kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu”–na ni wajibu wa mwalimu kuwawezesha watu kuelewa na kupokea neno hili” (J. Rodman Williams, Renewal Theology: Theology Systematic from a Charismatic Perspective , Buku la 3: The Church, the Kingdom and Last Things , Grand Rapids: Zondervan, 1996, uk. 180-81). 4. “Katika 1 Kor. 12:28 didaskalos inatajwa kama ofisi ya tatu ya karama tatu zinazohusiana (pamoja na mitume na manabii). Watu waliohudumu katika ofisi hii walikuwa na kazi ya kuelezea imani ya Kikristo kwa wengine na kutoa ufafanuzi wa Kikristo wa Agano la Kale.... Andiko la Yak. 3:1, likionya dhidi ya kufurika kwa watu katika ofisi ya kufundisha (ofisi
Made with FlippingBook Digital Publishing Software