Theolojia Katika Picha

/ 3 1 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)

na wachungaji na walimu) ingawa hawakuitwa hivyo hasa” (F. F. Bruce, “Waraka kwa Wakolosai, kwa Filemoni, na kwa Waefeso,” The New International Commentary on the New Testament , Buku la 10, Grand Rapids: Eerdmans, 1984, uk. 347). C. Muhtasari Wachungaji husimamia, kulea, kufundisha, na kulinda makusanyiko ya Kikristo na washirika wao. Lengo kuu la kazi ya uchungaji ni kumleta kila mtu “mkamilifu katika Kristo” ili jamii ya waamini itende na kunena ulimwenguni kama ambavyo Kristo angefanya. Kazi ya msingi ya mchungaji si “kufanya huduma” bali “kuwaandaa washirika kufanya huduma” kwa kuwazoeza katika Neno la Mungu na kwa kutambua karama zao za kiroho na kuwasaidia kuweka karama hizi katika matendo kwa ajili ya huduma na utume. Wamishenari wenye karama za kichungaji wana wajibu maalum wa kuwafundisha viongozi wazawa kuchukua hatamu ya kazi kutoka kwao.

III. Waalimu

A. Mazingatio ya Kiisimu didaskalos “Mwalimu” ( Kamusi ya Kiyunani ya Strong ya Maneno ya Agano Jipya ).

“Matendo 13:1 inarejelea neno didáskaloi kama waalimu na prophetai kama manabii. Kutokana na hili inahitimishwa kuwa katika kanisa la Kristo didáskaloi , waalimu wanaonekana kuwa na kazi maalum (Mdo. 13:1; 1 Kor. 12:23,29; Efe. 4:11; Yakobo 3:1). Hawa didáskaloi wanawajibika kwa grammateís (uwingi) waandishi wa Kiyahudi, na ni wa kutazamwa katika maana maalum kama wenye ufahamu wa wokovu wa Mungu na uwezo wa kuutafsiri (Mt. 13:52; Lk 2:46). Kwao uliangukia wajibu wa kutoa maarifa endelevu ya kusudi la Mungu la ukombozi, kazi ambayo, kulingana na Efe. 4:11, inaweza kuwa imeunganishwa na poimen , mchungaji, katika mtu mmoja. Hata hivyo, wataalam wa lugha wamejadili uhusiano sahihi kati ya waalimu na wachungaji katika kifungu hicho. Kuna kukua kwa makubaliano kuhusiana na dhana kwamba wachungaji ni kikundi kidogo ndani ya kundi kubwa la waalimu” (Spiros Zodhiates, The Complete Word Study Dictionary: New Testament , Chattanooga, TN: AMG Publishers, 1992).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software