Theolojia Katika Picha
3 1 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
B. Nukuu Husika za Kitheolojia 1. “Mitume na wainjilisti walikuwa na kazi maalum ya kupanda makanisa kila mahali; manabii, kuleta neno fulani la Mungu kwa ajili ya mazingira fulani. Wachungaji na waalimu walipewa karama kwa ajili ya kuwajibika na ujenzi wa kila siku wa kanisa” ( Francis Foulkes The Epistle of St. Paul to the Ephesians, Tyndale New Testament Commentaries , Grand Rapids: Eerdmans, 1956, uk. 119) . 2. “‘Wachungaji’ wanaweza kufananishwa kwa urahisi na wahudumu ambao mahali pengine wanaitwa ‘wazee’ ( presbyteroi ) au ‘maaskofu’ ( episkopoi lililotafsiriwa kama ‘walezi’ katika nukuu yetu iliyotangulia ya Matendo 20:28: ‘mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake’ [NEN] ambalo ni agizo lililotolewa kwa wazee na ‘mzee mwenzao’ katika 1 Pet. 5:2). (Inafaa kwamba agizo hili lihusishwe na mtume ambaye agizo lake la mwisho kutoka kwa Bwana, kulingana na Yohana 21:15-17, lilikuwa ‘Lisha kondoo wangu.’”) (F. F. Bruce, “Waraka kwa Wakolosai, kwa Filemoni, na kwa Waefeso,” The New International Commentary on the New Testament , Buku la 10, Grand Rapids: Eerdmans, 1984, uk. 348). 3. “Huduma ya mchungaji ni huduma ya upendo. Hakuna mwanadamu anayeweza kufanya huduma hii bila kuwa na moyo wa mchungaji kama kipawa kutoka kwa Mungu.... Yesu alionyesha kwamba tabia ya mchungaji wa kweli ni kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake... Mtu anapopewa moyo wa mchungaji wa kweli, anakuwa pale kwa ajili ya manufaa ya kundi bila kujali gharama binafsi.... Kazi za mchungaji ni tofauti lakini nyingi zinaweza kuwekwa chini ya vichwa vitatu vya jumla. Kwanza, mchungaji lazima asimamie na kulisha kundi la Mungu.... Pili, ana jukumu la kuwalinda na kuwaelekeza watu... Tatu, mchungaji lazima awe mwalimu wa Neno kwa kanuni na kielelezo” (Joe H. Cothen, Equipped for Good Work , Gretna, LA: Pelican Publishing, 1996, uk. 13-15). 4. “Pamoja na chochote kile ambacho karama ya uchungaji inaweza kuwa, karama hii ni kichocheo kinachokusudiwa kuchochea na kuachilia uwezo na utendaji wa karama za wale walio katika kundi” (Kenneth O. Gangel, Unwrap Your Spiritual Gifts , Wheaton, IL: Victor Books, 1983) , uk. 72). 5. “Mitume walihubiri injili kabla hawajaanzisha makanisa na kuwapa waongofu wao mafundisho zaidi; walikuwa kwa kweli wainjilisti (pamoja
Made with FlippingBook Digital Publishing Software