Theolojia Katika Picha

/ 3 1 1

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)

II. Wachungaji 1

1 Kwa sababu Paulo katika Waefeso 4:11 haweki kibainishi dhihirishi kabla ya neno “waalimu,” kumekuwa na mjadala kwa muda mrefu katika Kanisa ikiwa alikusudia kuzungumzia ofisi moja tu, “mchungaji “waalimu.” John Calvin anaelezea mjadala huo anaposema, “Wengine wanaamini ‘Wachungaji na Waalimu’ inaashiria ofisi moja.... Chrysostom na Augustine wana maoni haya.... Kwa sehemu nakubaliana nao, kwamba Paulo anazungumza bila kubagua kuhusu wachungaji na waalimu kuwa ni wa tabaka moja, na kwamba jina mwalimu, kwa kiasi Lakini silioni hili kama sababu ya kutosha ya kuchanganya ofisi mbili ambazo binafsi naona kuwa zinatofautiana. Kufundisha, bila shaka, ni wajibu wa wachungaji wote; lakini ili kudumisha mafundisho yenye uzima kunahitajika kipawa cha kufasiri Maandiko, inawezekana mtu kuwa mwalimu lakini asiwe na sifa za kuhubiri” (”Epistle to the Ephesians,” Calvin’s Commentaries, vol. XXI, Grand Rapids: Baker, 1981, uk. 279 -280). Andiko hili linaungana na Calvin katika kuunga mkono uwezekano wa ofisi mbili tofauti, huku likizingatia kwamba katika utendaji mara nyingi ofisi zote mbili huunganishwa katika mtu mmoja. fulani linawahusu wachungaji wote. mwalimu” au ofisi mbili kwa maana ya “wachungaji” na

A. Mazingatio ya Kiisimu Poimeni “Mchungaji” (kihalisia au kitamathali) ( Kamusi ya Kiyunani ya Strong ya Maneno ya Agano Jipya ). “Mchungaji, ni neno lenye chimbuko lake katika familia ya lugha zinazozungumzwa katika sehemu za Ulaya na Magharibi mwa Asia, ambalo hutumiwa mara kwa mara katika maana za kisitiari: kiongozi, mtawala, kamanda. . . .Plato anatukumbusha juu ya matumizi ya kidini ya neno hilo anapolinganisha watawala wa serikali ya jiji na wachungaji wanaochunga kundi lao” (E. Beyreuther, The New International Dictionary of New Testament Theology , Buku la 3, Colin Brown, Mhariri Mkuu, Grand Rapids: Zondervan, 1986, uk. 564). “[Mchungaji, Shepherd ] ni neno linalopatikana mara kwa mara katika Maandiko. Wakati fulani neno “mchungaji” [pastor] hutumiwa badala yake (Yer. 2:8; 3:15; 10:21; 12:10; 17:16). Neno hili linatumiwa kama lugha ya picha kuwakilisha uhusiano wa watawala na raia wao na uhusiano wa Mungu na watu wake (Zab. 23:1; 80:1; Isa. 40:11; 44:28; Yer. 25:34, 35; Nah. 3:18; Yoh. 10:11, 14; Ebr. 13:20; 1 Pet. 2:25; 5:4). Kazi za mchungaji katika nchi iliyo wazi kama Palestina zilikuwa ngumu sana. “Asubuhi na mapema alilitoa kundi kutoka zizini, akilitangulia mpaka mahali ambapo alipaswa kulilisha. Hapo aliliangalia mchana kutwa, akihakikisha kwamba hakuna kondoo hata mmoja atakayepotea, na ikiwa kondoo yeyote alikwepa lindo lake kwa muda fulani na kutangatanga mbali na wengine, alimtafuta kwa bidii mpaka ampate na kumrudisha. Katika nchi hizo kondoo huhitaji kunyweshwa maji mara kwa mara, na kwa sababu hiyo mchungaji alipaswa kuwaongoza ama kwenye kijito fulani chenye maji au kwenye visima vilivyochimbwa nyikani na kuwekewa mabirika. Usiku alilileta kundi nyumbani kwenye zizi, akiwahesabu walipokuwa wakipita chini ya fimbo mlangoni ili kujihakikishia kwamba hakuna aliyepotea. Wala kazi zake hazikuisha na machweo ya jua. Mara nyingi ilimbidi alinde zizi wakati wa giza dhidi ya shambulio la hayawani-mwitu, au majaribio ya hila ya mwizi anayewinda” ( ona 1 Sam. 17:34) (“Shepherd,” Easton’s Bible Dictionary ).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software