Theolojia Katika Picha

3 1 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)

mchungaji na mwalimu huanza, ya kuwaelekeza zaidi katika mambo ya Kristo na kuwajenga katika imani” (J. M. Gray, The International Standard Bible Encyclopedia , Toleo la 2, Geoffrey W. Bromily, Mhariri mkuu. Grand Rapids: Eerdmans, 1982, uk. 204). C. Muhtasari 1. Kama ilivyo kwa huduma za kitume na kinabii, kazi kuu ya ofisi ya uinjilisti ni ya kuzunguka na ya kimishenari. Ofisi ya uinjilisti inatambua kwamba ingawa Ukristo unaenea kwa kawaida kupitia oikos (familia na marafiki) za watu waliookoka, mara nyingi hukutana na vikwazo (utamaduni, jiografia, dini zinazoupinga, n.k.) ambavyo uenezaji wa kawaida wa Injili hauwezi kuvishinda haraka. Ni kazi ya kipekee ya mwinjilisti kufungua uwanja ili kutengeneza mazingira yanayoweza kuifanya Injili kuenea kwa njia za kawaida zaidi. 2. Karama ya uinjilisti huhakikisha kwamba neema maalum ya hekima na nguvu ya Roho ipo ili mwinjilisti awe na ufanisi usio wa kawaida katika kuvuta usikivu wa watu kwa Injili, hata katika mazingira ya uhasama. Ofisi ya mwinjilisti inamweka huru mtu mwenye karama hiyo kwa ajili ya huduma ya kuzunguka maeneo mengi kwa namna ambayo inaweza kudhaminiwa na kanisa kubwa zaidi, na kumpa mtu huyu mwenye kipawa jukumu maalum la kuwachochea na kuwaandaa wainjilisti katika makanisa ya mahali yaliyoanzishwa kupitia huduma ya kimishenari, kwa sababu, kama zilivyo ofisi zote za Waefeso 4:11, ofisi ya mwinjilisti pia ipo ili “kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma.” 3. Ingawa mwinjilisti anafanya kazi tofauti katika utume, kazi ya mwinjilisti haipaswi kutenganishwa na kazi ya upandaji makanisa. Hili linaonekana wazi katika Matendo 8, ambapo mafanikio ya uinjilisti wa Filipo huko Samaria yalifikia kilele katika ziara ya mitume waliowathibitisha waongofu, kuwabatiza waamini wapya, kuhakikisha kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu unaeleweka na kupokelewa na jumuiya hii mpya ya Wakristo, wakitumia kuwekea mikono kama namna ya kutambua rasmi uhalali wa waongofu hawa wapya, na kuweka katika vitendo mafundisho na nidhamu ya kanisa (kumsahihisha Simoni aliyekuwa mchawi), na kupanua kazi ya utume kwa kuhubiri katika miji mingine ya Wasamaria. Kwa maneno mengine, huduma ya wainjilisti ni hatua ya kwanza katika mchakato wa upandaji kanisa na ufuasi, si ofisi inayojitegemea au iliyokusudiwa kutumia karama zake za huduma kwa namna ya kujitenga.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software