Theolojia Katika Picha
/ 3 0 9
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
[Amsterdam 2000] ulikuwa ni mkusanyiko wa waumini wa kiinjili wa dunia nzima walio katika kazi ya utume, ulioitishwa na Chama cha Kiinjilisti cha Billy Graham ukiwalenga kimahususi wainjilisti wasafirio na wajibu wao katika utume wa ulimwengu]). 3. “Itaonekana basi kwamba ingawa mitume walikuwa wainjilisti, si wainjilisti wote walikuwa mitume. Tofauti hii inathibitishwa katika Waefeso 4:11, ambapo ofisi ya mwinjilisti inatajwa baada ya “mtume” na “nabii,” na mbele ya “mchungaji” na mwalimu. Kutokana na kifungu hiki ni wazi kwamba karama ya uinjilisti ilikuwa ni karama ya pekee ndani ya kanisa la Kikristo; na ijapokuwa Wakristo wote bila shaka walifanya kazi hii takatifu, kwa kadri walivyopata fursa, kulikuwa na baadhi ya watu ambao walikuwa wameitwa na kukirimiwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya kazi hii.” (D.B. Knox, “Evangelist,” New Bible Dictionary , Toleo la 2, J. D. Douglas na wengine, wahariri. Leicester, England-Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1982, uk. 356-57). 4. “Watu kama hao hawakuitwa mahususi kutumikia kusanyiko fulani, bali walizunguka mahali na mahali, wakitangaza Injili kwa watu popote walipopata nafasi.... Wainjilisti hutangaza Injili ya Yesu Kristo kwa namna ambayo inakuwa habari njema kwa wasikilizaji. Wasikilizaji huitikia na kuwa wafuasi waaminifu na waliojitoa kikamilifu kwa Yesu Kristo. Mwinjilisti pia ana upako maalum “kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe” (Efe. 4:12). Kuwatambua rasmi watu kama hao ndani ya kusanyiko na kanisa kwa ujumla huwezesha mchakato wa kuwaleta watu katika imani ndani ya Kristo” (Harley H. Schmitt, Many Gifts, One Lord , Fairfax, VA: Xulon Press, 2002, uk. 77) 5. “Mhubiri wa Kibiblia bila shaka ni mjumbe kwa wasiofikiwa na Injili, akiandaa njia kwa ajili ya mchungaji na mwalimu katika huduma yake ya kudumu zaidi ndani ya kanisa” (Lewis Sperry Chafer, True Evangelism, Grand Rapids: Zondervan, 1967, uk. 6). 6. “Itaonekana kwamba, kama utaratibu katika huduma, kazi ya mwinjilisti inatangulia ile ya mchungaji na mwalimu, jambo ambalo linaendana na sifa za kazi ambayo kila mmoja bado anatambulika kuwa anaifanya. Mwinjilisti hana mahali pa kudumu, lakini anazunguka-zunguka katika maeneo mbalimbali, akihubiri injili kwa wale ambao hawajaisikia. Hawa wanapoongoka na kuungamanishwa na Yesu Kristo kwa imani, kazi ya
Made with FlippingBook Digital Publishing Software