Theolojia Katika Picha

3 0 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu Zinazopatika katika

Waefeso 4:11 Mch. Terry Cornett, M.A., M.A.R.

I. Wainjilisti

A. Mazingatio ya Kiisimu Euagglistes

“Mhubiri wa Injili” ( Kamusi ya Kiyunani ya Strong ya Maneno ya Agano Jipya ) “Neno lililotafsiriwa katika Agano Jipya kama ‘mwinjilisti’ ni nomino inayotokana na kitenzi euangelizomai ‘kutangaza habari’ na kwa kawaida hutafsiriwa . . . kama ‘hubiri injili’” (D.B. Knox, “Evangelist,” New Bible Dictionary , Toleo la 2, J. D. Douglas na wengine, wahariri. Leicester, England Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1982, uk. 356). “Neno la Kiyunani la mwinjilisti (Efe. 4:11) ni muunganiko wa maneno mawili. Neno la kwanza la Kiyunani ambalo ni eu linamaanisha “nzuri, njema, ~a wema, sahihi, ~a kufaa.” Neno la pili aggelos linamaanisha “mjumbe, aliyetumwa, malaika wa Mungu.” Neno Mwinjilisti linatoa maana ya mtu ambaye ni mjumbe mzuri, mjumbe anayekuja kuleta habari njema–habari ambazo zitaijaza mioyo ya wasikilizaji furaha na shukrani” (Harley H. Schmitt, Many Gifts, One Lord , Fairfax, VA: Xulon Press, 2002, uk. 76). B. Nukuu Husika za Kitheolojia 1. “Mhubiri wa Injili aliujua ujumbe wa Injili vizuri na aliweza kuufafanua, kama mwinjilisti Filipo alivyomfanyia towashi.... Hapo awali, neno euaggeliste liliashiria shughuli badala ya ofisi. Kunaweza kuwa na tofauti ndogo kati ya mtume na mwinjilisti, mitume wote ni wainjilisti, lakini si wainjilisti wote ni mitume” (Spiros Zodhiates, The Complete Word Study Dictionary: New Testament , Chattanooga, TN: AMG Publishers, 1992, uk. 670-671). 2. “Kila mkristo ameitwa kufanya sehemu yake katika kutimiza Agizo Kuu la Yesu, lakini waamini wengine wana wito maalum na karama maalum kwa ajili ya kumtangaza Kristo na kuwaongoza wengine kwake. Hawa tunawaita wainjilisti, kama wanavyoitwa katika Agano Jipya” (Tamko la Amsterdam, lililochapishwa katika Christianity Today, Agosti 7, 2000,

Made with FlippingBook Digital Publishing Software