Theolojia Katika Picha
/ 3 1 9
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
katika mapokeo mengine mahubiri na unabii huchukuliwa kuwa kitu kimoja). Uongozi huu wa kinabii na maendeleo yake unaweza kutokea kwa namna tofauti tofauti kuhusiana na jinsi wahusika wanavyotambua, wanavyotathmini na kutii sauti ya Roho Mtakatifu inayoongoza katika kweli yote. Wabaptisti, Wapentekoste, Wamennonite, na Wapresbiteri wana mapokeo tofauti sana kuhusu lugha na njia zinazotumika katika mchakato huu lakini wote wanachukulia kwa uzito kwamba Kanisa lazima lisikie hasa kile ambacho Mungu anawaambia katika wakati wa sasa. A. Mazingatio ya Kiisimu Apostolos Mwakilishi ; hasa, balozi wa Injili ; kwa lugha rasmi kamishna wa Kristo ( Kamusi ya Kiyunani ya Strong ya Maneno ya Agano Jipya ). “ Mwakilishi, mjumbe, mtu aliyetumwa kwa amri .... linatumika hasa kwa wale wanafunzi kumi na wawili ambao Kristo aliwachagua kutoka katika umati wa wafuasi wake kuwa waandamani wake wa kudumu na watangazaji wa kuwatangazia wanadamu Ufalme wa Mungu. . . . Kwa maana pana zaidi jina hilo linahamishiwa kwa waalimu wengine mashuhuri wa Kikristo; kama Barnaba, Mdo 14:14, na labda pia Timotheo na Silwano,” (1 The. 2:7, rej. pia Rum. 16:7). (Joseph Henry Thayer, A Greek-English Lexicon of the New Testament , Grand Rapids: Baker, 1977, uk. 68). Mamlaka za lugha kwa ujumla zinakubali kwamba kuna mambo machache yanayofanana kati ya jinsi dini ya Kiyahudi ya Uyunani wa kale au ya kipindi cha kati ya AK na AJ ilivyotumia neno mtume na umuhimu ambao neno hilo lilikuja kuwa nao katika huduma ya Yesu au Kanisa la baada ya Pentekoste. 3 B. Nukuu Husika za Kitheolojia 1. [Paulo] basi, kwa ujumla wake, anawaita wale waliopo mahali hapa [Rum. 16:7] 4 Mitume, waliopanda makanisa kwa kubeba hapa na pale fundisho la wokovu . . .” (John Calvin, “Romans,” Calvin’s Commentaries , buku la 19, Grand Rapids: Baker Book House, 1981, uk. 546). 2. “Vyeo ‘mtume’ na ‘nabii’ vinatokea katika Agano Jipya vikiwa na maana pana na finyu. Wakati mwingine neno ‘mtume’ hujazwa na maana ya
V. Mitume
3 Tazama, kwa mfano, makala juu ya “Apostolos” katika Kamusi ya Theolojia ya Agano Jipya [Theological Dictionary of the New Testament], buku la 1, Gerhard Kittel, mhariri. Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans, 1964, uk. 398-420.
4 Warumi 16:7 inawataja Androniko na Yunia, ambao hawakuwa sehemu ya wale kumi na wawili,
lakini walionenwa kuwa mitume na Paulo.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software