Theolojia Katika Picha
3 2 0 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
uchaguzi na mamlaka maalum; katika maana hizi limetumiwa kwa habari ya wanafunzi kumi na wawili wa Yesu na Paulo. Katika matukio mengine linatumiwa kwa maana pana zaidi: kila shahidi wa Kristo aliyefufuka na yeyote aliyeidhinishwa na kanisa kwa ajili ya kazi ya umishenari anaweza kuwa na cheo hicho pia (Mt. 10:1-5; Gal. 1:1, 17, 19; 1Kor. 9:1-2; 2 Kor. 8:23)” (Karl Barth, Ephesians 4-6, Garden City, N.Y.: Doubleday & Co., 1974, uk. 314 iliyonukuliwa katika kitabu cha Harley H. Schmitt, Many Gifts, One Lord , Fairfax, VA: Xulon Press, 2002). 3. “[Mtume] ni neno la kina kwa ajili ya ‘wabeba ujumbe wa AJ.’ Jina hilo linatumika kwanza kwa lile kundi la thenashara kumi na wawili, yaani, mitume wa kwanza.... Hata hivyo jina hilo pia linatumiwa kwa wamishenari Wakristo wa kwanza au wawakilishi wao mashuhuri zaidi, kutia ndani wengine ambao hawakuwa hata wa vikundi vipana zaidi vya wanafunzi” (Gerhard Kittel, mhariri, Theological Dictionary of the New Testament , Buku la 1, Grand. Rapids: Wm. B. Eerdmans, 1964, uk. 422). 4. “Neno mitume linaashiria makundi matatu tofauti ya watu. Hapo awali, ni thenashara wa kwanza tu (maana yake “wanafunzi”) wa Yesu walioitwa mitume (maana yake “wale waliotumwa wakiwa na agizo”). Baadaye, jina hilo walipewa wamishenari waliohusika katika upandaji makanisa ambao pia walikuwa mashahidi walioshuhudia ufufuo wa Kristo, kama vile Paulo mwenyewe (1Kor. 9:1-1) na kundi la wafuasi wa Yesu zaidi ya wale Kumi na Wawili (1Kor. 15:5, 7). Hatimaye, jina hilo lilienea kwa watu ambao hawakuwa wamemwona Kristo kamwe lakini walihusika pamoja na mitume katika jitihada za umishenari wa upainia—Apolo (1 Kor. 4:6,9); Epafrodito (Flp. 2:25); Silwano na Timotheo (1The.1:1, taz. 2:6). Ufafanuzi wa ‘mitume’ kama mojawapo ya karama za juu zaidi zinazohitajika kunatoa uthibitisho wa kuendelea kupatikana kwa huduma hii kwa watu wenye sifa na vigezo (1Kor. 12:28, taz.31). Wakristo wa Korintho wangeweza kutamani kuwa mitume, manabii, au waalimu. Neno mtume bado lilitumika kwa maana hii pana katika maandiko ya kipindi cha baada ya mitume, yaani Didache ” (Gilbert Bilezikian, Beyond Sex Roles: What the Bible says about a Woman’s Place in Church and Family , Grand Rapids, MI: Baker Book House, 1986). 5. “Waumini wengi wa kinjili hujisikia vibaya sana kutumia neno mtume kuelezea ofisi au kiongozi yeyote katika kanisa leo. Je, inawezekana kwetu, hata hivyo, kufikiria kuhusu kutofautishwa kwa karama na ofisi baada
Made with FlippingBook Digital Publishing Software