Theolojia Katika Picha
/ 3 2 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
ya karne ya kwanza? Badala ya kuamini kwamba karama hii inahusu tu historia ya kanisa la kwanza, je, hatuwezi kuitambua maana pana ya umbo la kitenzi apostello ? Je, haiwezi kuwa kwamba katika kipindi cha kati ya karne ya 1 na ya 20 Roho Mtakatifu ametoa karama hii kwa watu wa Mungu katika kile ambacho tumekuja kukiita huduma ya kimishenari ? . . . Wengi wamechagua kufungia karama kadhaa za kiroho katika karne ya kwanza, ili kuepuka kutoa maelezo fulani yanayoweza kuhitajika kuhusu uwepo wa karama hizo katika kanisa leo. Ningependelea kumpa Roho Mtakatifu mawanda mapana zaidi ya kutoa karama yoyote katika Mwili wa Kristo katika enzi yoyote kama anavyoona inafaa. Inaonekana ni salama kabisa kusema kwamba ofisi ya mitume ilikusudiwa tu kwa ajili ya kuanzishwa kwa kanisa la Agano Jipya. Lakini. . .tunaweza kuhesabiwa kuwa na haki katika kuona ushahidi wa “utume” sio tu kama karama, bali kama karama ambayo imetenda kazi ndani ya kanisa katika miaka yote ya historia yake” (Kenneth O. Gangel, Unwrap Your Spiritual Gifts , Wheaton, IL. : Victor Books, 1983, uk. 26-27). 6. “Kuna utofauti unaoweza kuonekana dhahiri kati ya huduma ya msingi ya mtume, yaani, utume, na huduma inayoendelea ya wengine wanaoitwa mitume. Kwa maana hii pana mtume ni mtu aliyetumwa, aliyeagizwa , na kwa hiyo hajafungamanishwa na eneo au kanisa fulani. Hana mamlaka ya mtume wa msingi wala maneno yake hayajavuviwa kwa kiwango sawa na cha mtume wa msingi. Mtume kama huyo anafanya kazi kwa namna isiyofungamana na eneo moja tu la kijiografia, lakini hafanyi kazi kwa kujitegemea. Ana kituo katika kanisa, akiwakilisha kanisa fulani, lakini huduma yake kwa sehemu kubwa inaenda zaidi ya mipaka hiyo. Mitume kama hao daima ni muhimu kwa maisha ya kanisa ambalo linatambua wito wake wa kufikia maeneo yaliyo nje ya mipaka yake katika utume wa injili” (J. Rodman Williams, Renewal Theology: Systematic Theology from a Charismatic Perspective , Buku la 3: The Church, the Kingdom Last Things , Grand Rapids: Zondervan, 1996, uk. 169-70). 7. “Neno hilo mara kwa mara hutumika kwa maana pana katika AJ kwa watu wenye karama, neema, kazi na mafanikio ya kitume. Ndivyo ilivyokuwa hasa kwa Barnaba, ambaye alitumwa pamoja na Paulo (Mdo. 13:3; 14:4, 14). Vile vile mtu bado anakutana na semi kama Judson, mtume wa Burma” (“Apostle,” The Westminster Dictionary of the Bible , John D. Davis, mhariri. Philadelphia: The Westminster Press, 1944, uk. 36).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software