Theolojia Katika Picha
3 2 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
8. “Moja ya kazi kuu—yaani, kazi ya msingi–ya mtume (katika matumizi maalum ya Kikristo ya neno hilo) ilikuwa kuhubiri Injili. Mitume, kama tabaka la kihuduma katika kanisa, hawakuendelea zaidi ya enzi ya mitume, hata hivyo kazi mbalimbali walizozifanya hazikuisha kwa kuondoka kwao, bali ziliendelea kufanywa na wengine, hasa wainjilisti na wachungaji na waalimu walioorodheshwa hapa [katika Waefeso 4:11] . . . Mitume walihubiri Injili kabla hawajaanzisha makanisa na kuwapa waongofu wao mafundisho zaidi; walikuwa kwa kweli wainjilisti (na wachungaji na waalimu) ingawa hawakuitwa hivyo hasa” (F. F. Bruce, “Waraka kwa Wakolosai, kwa Filemoni, na kwa Waefeso,” The New International Commentary on the New Testament , Buku la 10. Grand Rapids: Eerdmans, 1984, uk. 346-347). 9. “Neno mtume lina maana ya mtu aliyetumwa , na linatumika kwa wengine pamoja na wale kumi na wawili wa asili. Leo, mtume ni mmishenari anayefikia maeneo mapya” (Avery Willis, Jr. Biblical Basis of Missions, Mfululizo wa Mafundisho ya Kibaptisti, Nashville: Convention Press, 1979, uk. 108). 10. “Kwa kuzingatia [Waefeso] 2:20 na 3:5 na ukweli kwamba Paulomwenyewe alitenda kazi kama mtume na nabii, majina matatu ya kwanza [mitume, manabii na wainjilisti] kimsingi yanarejelea huduma za kuzunguka kati ya makanisa ya kwanza, ingawa kwa habari ya manabii na wainjilisti ni zaidi ya hilo. Watenda kazi wa kusafiri walianzisha makanisa kwa kueneza injili na kuyajenga kupitia maneno ya kinabii. Kunaweza kuwa na swali kidogo ikiwa huu ndio uelewa wa neno “mtume” katika nyaraka za Paulo” (Gordon D. Fee, God’s Empowering Presence , Peabody, MA: Hendrickson, 1994, uk. 707). C. Muhtasari Wazo kwamba maana pana ya utume iliyotumiwa katika nyaraka za Paulo na neno la kisasa “mmishenari” kiutendaji yanalingana lina uungwaji mkono mkubwa katika elimu ya sasa ya Biblia na ya kitheolojia na ufahamu huu kwa kawaida (ingawa sio ulimwenguni kote) unapatikana katika mirengo yote miwili ya kitheolojia ya Kiinjili, yaani mrengo wa Kimageuzi ( Reformed ) na ule wa Kiamenia ( Arminian ). 5 Katika maana hii pana karama ya kitume inahusishwa sana na wale walioitwa katika huduma ya utume wa upandaji makanisa kwa kuzungukia maeneo yasiyofikiwa.
5 Vivyo hivyo, Ukatoliki wa Kirumi ambao unakuza cheo cha utume kwa njia ambayo Waprotestanti hawafanyi (yaani, maaskofu wa kanisa ni waandamizi wa Mitume kwa ile maana finyu ya neno hilo na wanatumikia ofisi yao kwa mamlaka kupitia mtiririko wa moja kwa moja wa urithi wa kitume), hata hivyo, pia wanatunza utofauti kati ya maana finyu na pana ya neno “mtume.” Hivyo, Kanisa Katoliki linafundisha kuwepo kwa aina pana zaidi ya huduma ya kitume katika maana pana ya umishenari na huduma ya kuwafikia wasiofikiwa wakisema, “Kwa hakika, tunaita utume ‘kila utendaji wa Mwili wa Fumbo’ unaolenga ‘kueneza Ufalme wa Kristo duniani kote’” (Katekisimu ya Kanisa Katoliki, Liguori, MO: Liguori Publications, 1994, uk. 229).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software