Theolojia Katika Picha
/ 3 2 3
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Muhtasari wa Kitheolojia wa Karama za Kuwakamilisha Watakatifu (muendelezo)
Licha ya hayo, hata hivyo, pengine ni bora zaidi kuzingatia ukomo wa wazo la “Ofisi ya Kitume” kwa maana finyu zaidi ya wale Kumi na Wawili (Mathiasi akichukua nafasi ya Yuda) pamoja na Paulo. Kwa hivyo, umishenari ni neno bora zaidi kuliko mtume kwa wapanda makanisa wa kisasa wa tamaduni mbalimbali kwa sababu linahifadhi mantiki ya kilugha ya mtu aliyetumwa katika umisheni bila kulikengeusha kwa kulifananisha na mamlaka maalum iliyobebwa na Mitume wa kwanza ambao walitumwa moja kwa moja na Bwana Aliyefufuka. Hata hivyo, inapaswa kutambuliwa kwamba asili ya kazi ya umishenari ni kuwa “mitume wadogo” wakitoa ushuhuda kwa Kristo na kutumia mamlaka katika uanzishaji wa makusanyiko yao ndani ya mipaka ya Maandiko. Mitume wa kwanza waliweza kuongea kwa mamlaka kwa Kanisa zima, wamisionari wanaweza kusema kwa mamlaka kwa makanisa waliyoyapanda ndani ya mipaka ya Maandiko. Hatimaye, kwa Mitume na wamishenari, suala la mamlaka si la kutawala kama mabwana bali ni kukuza na kuendeleza makusanyiko na viongozi ambao wanaweza kumsikia na kumtii Kristo. 6 Karama ya kimishenari (ya kitume), ikifafanuliwa kwa njia hii, inaonyesha kwamba: • mtu anahisi wito wa “dharura” kwa ajili ya wasiofikiwa, • mara kwa mara atasonga mbele kuyaendea makundi mapya ambayo hayajafikiwa, • atajizoeza haraka kuendana na tamaduni mpya ili kuvuna watu wengi iwezekanavyo; • na, atainua viongozi kwa ajili ya makanisa mapya anayopanda ili kwa njia hii yeye (mmishenari) aweze kutumika kama “mchungaji wa wachungaji.”
6 Msingi wa mamlaka yoyote halali ya Kikristo ni uwezo wake wa kujenga (taz. 2Kor. 10:8). Kiini na mantiki ya mamlaka ni kubariki, si kutawala kiimla. Hata lugha ya moja kwa moja ya “kujitiisha kwa viongozi” katika Waebrania 13:17 imejengwa juu ya msingi wa kwamba kujitiisha huko kutaleta “faida” kwa mfuasi. Wakristo wananyenyekea kwa viongozi kwa sababu wao ni kipawa cha Mungu kwa ajili ya kujenga na kulinda kusanyiko. Kiongozi yeyote wa Kikristo anayedai kuwa na mamlaka ambayo hayahusishi utii kwa Kristo, kujitiisha kwa Maandiko, kukua kwa Kanisa la Kristo, au kuwajenga washirika wake, hatumii tena mamlaka ya kibiblia. Paulo ameliweka wazo hili wazi katika sehemu zinazofuata anapoandika kwamba “kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke” kunakusudiwa kusababisha “mwili wa Kristo ujengwe” (Efe. 4:13).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software