Theolojia Katika Picha

/ 4 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Hadithi, Thilojia, na Kanisa (muendelezo)

hadithi ambazo watu waliziishi na kusimuliana mmoja na mwingine, ambazo tumekuja kuzieleza kama ni kushangilia kwa siri na mambo ya ajabu ya Mungu au zimekuja kuitwa tu sakramenti. Hadithi (neno) sherehe(tafrija) na sherehe za kidini (sakramenti) zote zinakwenda pamoja. Bila shaka inaweza kutokea, na imeshatokea kwamba sherehe ya kinini inaweza kupoteza muunganiko wake wa hadithi, kupitia kufanyika kama taratibu za kawaida, kuboa, na kurudia mara kwa mara. Hii ikitokea watu kiuhalisia wanaendelea na sherehe hizo kutokana na mazoea, lakini, hawakumbuki hadithi ilikuwa imeshikamana na nini au inaelezea nini. Ili kuhuisha au kuingiza upya matukio katika sherehe hizi za kidini, lazima turudi nyuma na kukumbuka vizuri hadithi hiyo. Kufanywa upya kwa Kanisa kimsingi ni moja ya mazoezi ya kulikamilisha jambo hili.

Pendekezo la Kumi: Hadithi ni historia

Kwa sababu hadithi zinamwisho unaoruhusu mawazo zaidi, zenyewe haziwezi kuwa au hazitakiwi kufanywa kuwa fasihi. Hadithi zina uhai wa aina yao na kila kipindi kinatoa au kuongeza uhai huo kwa njia ya kuwa pamoja na kuhusiana. Matokeo yake ni kuwa na utajirisho wa kina. Historia ni daraja ambalo kwa hilo tunaitazama hadithi kutoka katika aina zake zote na katika masuala yake yote ya kweli. Kimsingi, historia inaiokoa hadithi kutoka katika hatari ya ibada ya sanamu na kutokuwa na umuhimu tena.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software