Theolojia Katika Picha

4 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Hadithi, Thilojia, na Kanisa (muendelezo)

Au tunaweza kuiweka kwa namna hii: Theolojia inachipuza kwa sababu mara zote huwa kuna vitu vya zaidi katika hadithi kuliko vile ambavyo msimuliaji eidha amevigungua au amekusudia kusimulia. Tuna mfano halisi katika kitabu cha Injili ya Yohana (11.49-52): «Mtu mmoja miongoni mwao, kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule,akawaambia ‘ninyi hamjui neno lolote; wala hamfikiri ya kwamba ya faa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima’ kisha Yohana anaendelea na kutoa tafakari yake na maana zaidi kuhusiana na maneno haya(theolojia): «Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo, wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wa moja. Wakati na kutazama yaliyotangulia mara nyingi kunafunua mawazo muhimu zaidi katika hadithi. Theolojia inashikilia hili na inalifunua. Theolojia ina mizizi yake na inaenda sawa na hadithi. Hadithi za Yesu zenyewe zinatofautiana na bila shaka zina akisi mila tofauti. Hata usomaji wa kawaida wa vitabu vinne vya Injili unaonyesha hili. Na kwasababu hili liko hivyo, basi tunatarajia mila hizo tofauti za hadithi zitatupa aina mbalimbali za theolojia. Hakuna mfumo mmoja uliotengenezwa ili kwamba uwe ndio huo tu. Hadithi za kawaida zenyewe, ambazo pia, sio tu zinaruhusu mawazo zaidi mwishoni bali pia zimewekwa katika hali ya dhana na katika marejeo ya mfumo wa nyakati zao. Kumekuwa na kutaendelea kuwa na mifumo mingi ya theolojia katika Kanisa. Ingawa kumekuwa na msukumo katika nyakati hizi za sasa wa kuifanya mifumo yote iwe mmoja, katika historia ya Kanisa kumekuwa na uvumilivu sana juu ya utofauti uliopo katika mifumo hii. Lazima tukumbuke kwamba maisha ya Yesu yalianza kabla ya tafakari kumhusu yeye. Hii ndio njia ya kuhifadhi maisha hayo ambayo yalikuwepo kabla ya kuyafikiri, na hadithi hiyo ilikuja kabla ya theolojia. Maisha ya Yesu yalikuwa halisi, kama tulivyoona, yakiwekwa katika hadithi, lakini ni lazima pia izingatiwe kwamba yaliingizwa sambamba katika sherehe za kidini na sikukuu mbalimbali. Ishara, matendo, utumiaji wa lugha ya mwili na alama pia zilikuwa sehemu ya hadithi nzima. Sherehe ya ibada yenyewe ni sehemu ya hadithi katika matendo. Hivyo mpaka hapo tunaweza tokea sherehe za kidini zinazoigiza upya kifo, mazishi na ufufuo wa Yesu. Paulo anaita hii ni ubatizo. Na kisha kulikuwa na chakula kwa ajili ya sherehe hizo katika kuumega mkate na kukinywea kikombe, ishara za matendo ya kutolewa kwa Yesu. Kiufupi, kulikuwa pia na Pendekezo la Nane: Hadithi zinazalisha theolojia nyingi. Pendekezo la Tisa: Hadithi zinatengeneza sherehe za kidini na sakramenti

Made with FlippingBook Digital Publishing Software