Theolojia Katika Picha

/ 4 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Hadithi, Thilojia, na Kanisa (muendelezo)

Pendekezo la Tano: Hadithi hutangulia na kuzalisha kanisa.

Hili tulilitazama Mwanzoni. Hadithi inakuwepo kwanza na kisha watu wanashawishiwa nayo, wanatazama uzuri wake, wanaitafakari, wanaihadithia upya, wanaihifadhi na kuisema kwa watu wengine(mila) pale ambapo watu wengi wanakuwa wameshawishiwa nayo, wameiamini na kuishangilia, hapo sasa una Kanisa.

Pendekezo la sita: Hadithi inamaanisha laumu.

Pendekezo hili ni matokeo ya kimantiki ya mapendekezo mawili yaliyotangulia: Kama una mila ambayo imejikita katika kuhifadhi na kueneza kiini cha hadidhi husika, na kama una Kanisa linaloishi sawasawa na hiyo na kusherekea hiyo hadithi kuu, basi wale walio katika kundi ambalo muda wowote linaweza kwenda kinyume kwa kiwango kikubwa na hadithi ya msingi ni lazima washughulikiwe. Hapa ni sehemu ya kawaida sana katika maisha yote. Hapa ndipo tunapata dini, serikali, au shutuma, karipio, na kutengwa. Uwanja mpana unaruhusiwa lakini siyo kwenda mpaka hatua ya kukinzana na kile ambacho hadithi inakisimamia. Makundi yenye msimamo hayawezi, kwa mfano; kuvumilia upinzani uliopitiliza. Bila shaka, kama historia ilivyoonyesha watu huwa wanakuwa wanajizuia sana kwa kile wanachokiamini kuwa mila ya «Kweli» Kuliko hali yake ya kuwa sahihi au la. Fundisho la msingi kwa mtu mmoja linaweza kuwa uzushi kwa mtu mwingine kutegemeana na nani ana mamlaka kuu zaidi. Lakini hilo sio hoja kubwa hapa. Hoja hapa ni kwamba pale ambapo hadithi inachipuza mila, na mila ikachipuza Kanisa, basi shutuma katika maeneo fulani inatokeza muda wowote. (Kimsingi, mapema sana kama tulivyoona katika kujifunza kutoka katika nyaraka za Paulo) katika Mila yetu ya kikatoliki hiki ndicho chanzo cha adhabu na kutengwa. Tafakuri na hitimisho kutoka katika hadithi za Yesu zilianza mapema sana katika Kanisa. Tunaliona hili katika Maandiko ya Mwanzo kabisa ya Kanisa, nyaraka za Paulo. Pale unapotafakari juu ya hadithi, unganisha matukio na kupata hitimisho,hapo tayari una theolojia. Tunaweza kuona hili kirahisi, kwa mfano katika njia ya imani kuhusiana na asili ya Yesu. Kwa namna ya kipekee sana hadithi inatuambia yeye ni mtu wa Mungu. Kama ni mtu wa Mungu basi labda yeye ndiye msemaji wake pia na labda yeye ndiye Neno lake. Na kama yeye ni Neno lake basi labda anauhusiano maalumu na Baba, na kama anauhusiano maalumu na Baba, labda yeye ni Mwana wake-kwa namna ya kipekee. Na kama ni Mwana wa Mungu, labda yuko sawa naye. Na kama yuko sawa naye labda yeye ni Mungu katika mwili. Theolojia ni kuweka vipande vidogo vidogo pamoja na kugundua hitimisho lenye mantiki zaidi kuliko lile ambalo lingeweza kufikiwa mwanzo. Pendekezo la Saba: Hadithi zinazalisha theolojia

Made with FlippingBook Digital Publishing Software