Theolojia Katika Picha
4 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Hadithi, Thilojia, na Kanisa (muendelezo)
Pendekezo la Tatu: Hadithi zinabaki kuwa za kawaida kwa kuzingatia hali iliyopo katika jamii husika. Tumeona katika sura ya kwanza ya kitabu hiki kwamba kila theolojia ni akisi ya hadithi za asili. Ili kupima theolojia, lazima mara zote turudi nyuma kwenye maandishi safi.(na namna kulivyokuwa kuenea kwake baadae). Kwa kiwango hiki hadithi za Biblia zitabaki ziku zote kuwa za kawaida. Kuna tahadhari kubwa sana, hata hivyo, wengine wanaweza kurudi nyuma na kutengeneza vinyago kutoka kwenye hadithi hiyo; kwa maana kwamba wanaweza wakachukulia kama maandishi ambayo yako hivyo siku zote, wakayatoa kutoka katika historia, kuja kwenye ulimwengu huu na kuyalazimisha kubaki katika hali ileile ya mwanzo. Hii ni kazi ya wanafasihi au watu wanahusika na tafsiri za maandishi na nyaraka mbalimbali. Mila zinatokea kutoka kwenye hadithi. Hiyo ndio asili ya hadithi ya muhimu na yenye mantiki, watu «wakivutiwa» na hadithi, shujaa wake au adui wake na ujumbe wake, hawahitaji tu kushirikisha uzoefu bali kushirikisha uzoefu ulio sawasawa na hadithi ya asili. Hivyo mila zinachipuka ambazo zinakuwa na kazi mbili: Kuhifadhi na kulinda. Kuhifadhi ni «Kukabidhi kwa wanaofuata» ambacho ndicho neno mila lina maanisha moja kwa moja. Kulinda inaweza kuhitaji maelezo zaidi kidogo. Kwa sababu hadithi hakika ni sitiari zilizopanuka zaidi, huwa mwisho wake bado unaruhusu mawazo zaidi. Zinaweza kubadilika na kubadilisha wahusika na usimulizi wake kirahisi. Taarifa majina, na maeneo yanaweza kuchukuliwa tofauti kwa hadhira na maeneo tofauti. Tunaligundua hili hata katika kipindi kifupi cha uandishi wa vitabu vinne vya Injili. Hata hivyo mpaka umewekwa ili kuzuia Mtu kwenda mbali zaidi lakini bado akawa sahihi kabisa kutokana na hadithi wa awali. Tukichuchukua mifano ya kidunia: Santa Claus anaweza kubadilika kwa karne zote kirahisi zaidi. Anaweza kuwa mrefu au mfupi, mwenye uso Mwanana au wenye mikunjo, aliyevaa nguo za zambarau au kijani, mnene au mwembamba kama muigizaji wa nafasi ya Ichabod Crane. Lakini Santa hawezi kamwe kuwa mnyanyasaji wa watoto. Ukizingatia kwamba alipokea kutoka kwa Mt. Nicholaus, aliyepokea kutoka kwa mtoto Yesu, aliyepokea kutoka kwa Baba wa vipawa vyote. Mila ya asili isingeweza kuruhusu muunganiko baina ya Santa na madhara yoyote wakati lengo lake kubwa ni wema na ukarimu. Katika kuendelea na hayo kuna sehemu mila ingeilinda sura hiyo kutoka kwenye mkanganyiko. Hadithi za Biblia kuhusu Yesu zinahimiza mchakato huohuo wa kulinda. Hapa ndipo Mila ya Kanisa inaingia. Na kwasababu hadithi za Yesu zinatofautiana, basi mila zinazotofautiana sio tu zitachipuka lakini pia zitakuwa halali kabisa. Pendekezo la Nne: Mila zinatokea kutoka kwenye hadithi.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software