Theolojia Katika Picha
/ 4 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Hadithi, Thilojia, na Kanisa William J. Bausch. Storytelling: Imagination and Faith . Mystic, Ct: 23rd Publications, 1984. K. 195-199.
Mpaka hatua hii katika kitabu chetu, ukitazama kwa makini, inaweza kuwa vyema kukiweka pembeni kidogo kwa muda na kuruhusu hadithi na kielelezo (hayo mengine hata hivyo yatarejeshwa tena, katika surambili zamwisho) na kuorodheshamapendekezo kumi ya asili ya kitheolojia. Zoezi hili natumaini halitakuwa zito wala gumu. Litatumika kama njia ya kupata maarifa zaidi, kwa ajili ya kueleweka na kuweka msisitizo kwa maana za kitheolojia ambazo zimetajwa hapa na kule katika sura zilizopita. Hivyo hii ni sura fupi sana na ni aina ya muhtasari wa kitheolojia, mtazamo wa jumla wa namna hadithi zinavyohusiana na theolojia na muundo wa Kanisa. Pendekezo la Kwanza: Hadithi zinatufahamisha kuhusu uwepo wa sakramenti. Hadithi zimetungwa kutulazimisha kufikiria uwezekano wa jambo. Kwa kigezo hicho zimewekewa misingi katika tumaini. Hata kwa mfano, hadithi ambayo ni ya kigeni kabisa, bado inafufua uwekano na kuinua matumaini yetu. Hadithi za kibiblia zinafanya vivyohivyo, ila ni kwa uwazi zaidi kidogo. Dhumuni lao kubwa ni kutushawishi kutazama zaidi ya mipaka yetu na hali ya vikwazo vyetu na kufikiri uajabu uliopo kwa namna ya ajabu. Hadithi zinatukumbusha kwamba kuchukulia mambo juu tunakofanya kila siku kunaweza fanya tuone mambo mengi ni mageni. Katika hadithi kama “Rumors of angels” na Grace abounding. Kama chura angeweza kuwa Mwana wa Mfalme, baharia aliyepotea akawa malaika, msafiri akawa Kristo, basi uumbaji wote ungekuwa na uwepo wa sakramenti ukielekeza kwenye hadithi ya “Something more.” Hadithi zinaonyesha kwamba hii inaweza tu kuwa ndivyo ilivyo.
Pendekezo la Pili: Hadithi mara zote huwa ni muhimu kuliko kweli.
Kweli, kuhusiana na hadithi, hazina madhara. Ni suala la ubunifu wa hadithi kupangilia kweli na kueleza habari njema kuzihusu. Kwa mfano,” Kweli” Ya msingi, kuhusu ufufuo kimsingi ina umuhimu kidogo katika maelezo yake na uthibitisho wake kama kauli ya Yesu wa Nazareti kufufuka kutoka kwa wafu, kuliko nafasi ya msingi ya tumaini. Kilicho muhimu ni matokeo ambayo hadithi ya ufufuo inatupa katika maisha yetu na mtazamo wetu juu ya uzima na kifo. La si hivyo, basi hiyo ni ripoti tu na sio injili.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software