Theolojia Katika Picha

/ 4 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Hapo Zamani za Kale Tamthiliya inayohusu ulimwengu mzima kupitia simulizi ya Kibiblia Mch. Dkt. Don L. Davis Kutoka milele hadi milele, Bwana wetu ni Mungu. Kutoka milele, katika fumbo lisilo kifani la uwepo kabla ya kuanza kwa wakati, Mungu wetu wa utatu alikaa katika fahari kamili ndani ya jamii ya milele kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ambaye ni MIMI NIKO, akionyesha sifa zake kamili katika uhusiano wa milele asihitaji cho chote kwa utukufu usio na kikomo, furaha na haiba, kulingana na mapenzi ya enzi yake, Mungu wetu, kwa mapenzi yake alikukusudia kuumba ulimwengu ambao ungedhihirisha fahari yake, na dunia ambayo ingeonyesha utukufu wake, na pale wanapishi watu aliowaumba kwa mfano wake, wakishiriki, ushirika wake naye, wakifurahia mwungano na yeye mwenyewe katika uhusiano yote haya kwa utukufu wake. Wakichochewa na tamaa ulafi na kiburi, wanadamu wawili wa kwanza waliasi dhidi ya mapenzi yake, wakidanganywa na mkuu wa dunia shetani, ambaye kwa njama yake ovu ya kuchukua nafasi ya Mungu kama mtawala wa vyote ulisababisha viumbe wasio na idadi wa kimalaika kupinga mapenzi matakatifu ya Mungu huko Mbinguni. Kupitia kutotii kwa Adamu na Eva, walijiweka wao na warithi wao katika mateso na mauti, na kwa uasi wao walivileta viumbe katika machafuko, mateso na uovu. Kutokana na dhambi na maasi mwungano kati ya viumbe na Mungu ulipotea, kwa sasa vitu vyote viko katika athari ya anguko kuu huo –mfarakano, utengano na hukumu unakuwa ukweli muhimu kwa vitu vyote. Hakuna malaika, mwanadamu au kiumbe, kinacho weza kutanzua tatizo gumu hili, na bila uingiliaji wa moja kwa moja wa Mungu, ulimwengu wote, dunia na viumbe vyake vyote vingeangania. Na, bado katika rehema na upendo wa huruma Bwana Mungu aliahidi kumtuma Mwokozi kuukomboa uumbaji wake. Katika agano la enzi la upendo, Mungu aliamua kuponya athari ya uasi wa ulimwengu kwa kumtuma shujaa, mwanae pekee, ambaye angechukua mfano wa wanadamu wawili walioanguka, kuingia na kupindua kutengwa kwao kutoka kwa Mungu, na kuteswa badala ya watu wote kwa dhambi yao na kutokutii kwao. Hivyo kwa agano lake la uaminiifu, Mungu akawa amejihusisha moja ka moja katika historia ya mwanadamu kwa ajili ya wokovu wao. Bwana Mungu hujishusha kupigania uumbaji wake kwa ajili ya kuurejesha, uumbaji, kuuzima uovu mara moja na kuweka watu ambamo mashujaa wake watatokea kuimarisha utawala wake katika ulimwengu huu mara nyingine. Akiwa kama Mungu mwenye enzi aliumba ulimwengu ambao hatimaye ungeliasi dhidi ya utawala wake.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software