Theolojia Katika Picha

4 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Hapo Zamani za Kale (muendelezo)

Kwa hiyo aliinua watu ambamo mtawala angetoka. Na kwa hiyo, kupitia Nuhu, anaokoa ulimwengu kutoka katika uovu wake wenyewe, kupitia Ibrahimu aliteua kabila ambalo kwalo mbegu ingetoka. Kupitia Isaka, aliendeleza ahadi kwa Ibrahimu, na kupitia kwa Yakobo (Israeli) alianzisha taifa lake, akalitambulisha kabila ambalo kwalo angetoka (Yesu) Kupitia musa, aliwaokoa watu wake kutoka kwenye mateso na akawapa agano lake la amri, na kupitia Yoshua, aliwaleta watu wkle katika nchi ya ahadi. Kupitia waamuzi na viongozi aliwasimamia watu wake kupitia kwa Daudi, anaweka agano kumleta mfalme kupitia kabila lake ambaye angetawala milele. Licha ya ahadi yake kupitia, watu wake hawakutimiza agano lake mara kwa mara. Ushupavu wao na kuendelea kumkataa Bwana kulipelekea kulifikisha taifa katika hukumu, uvamizi, kupinduliwa na utumwa. Kwa rehema anakumbuka agano lake na kuruhusu mabaki kurudi –kwa ahadi na hadithi kutimizwa. Kiasi cha miaka mia nne cha ukimya kilitokea bado katika utimilifu wa wakati Mungu alitimiza ahadi ya agano lake kwa kuingia katikaufalme huu wa maovu, mateso na mafarakano, kwa kufanyika mwili. Katika utu wa Yesu wa Nazarethi, Mungu alishuka chini kutoka mbinguni na kukaa kwetu, akidhihilisha utukufu wa Baba akitimiza matakwa ya sheria za Mungu, na kuonyesha uwezo wa ufalme wa Mungu kwa maneno yake na kazi zake na utoaji wa mapepo. Pale msalabani alilchukua uasi wetu, akaangamiza mauti, akamshinda ibilisi, na akafufuka, siku ya tatu kuurejesha uumbaji kutoka Anguko, kukomesha dhambi, magonjwa na vita, na kutupatia maisha yasiyo na mwisho kwa watu wote wanao kubali wokovu wake. Ni karibu tena karibu sana, atarudi kwenye dunia hii na kufanya vitu vyote kuwa vipya. Alipaa katika mkono wa kuume wa Baba, Bwana Yesu Kristo amemtuma Roho Mtakatifu katika dunia akifanya watu wapya waliotokana na wayahudi na watu wa mataifa –Kanisa wakiamriwa chini ya uongozi wake wakishuhudia katika neno na matendo habari njema ya upatanisho kwa viumbe vyote na wakisha maliza kazi yao, atarudi kwa utukufu kukamilisha kazi yake kwa uumbaji na viumbe vyote. Mara tu mapema atazima dhambi, uovu, mauti, na athari ya laana zote milele na kuurejesha uumbaji wote chini ya utawala wa kweli akifanya upya vitu vyote katika mbingu mpya na nchi mpya ambako watu wote na viumbe vyote vitafurahia amani ya utatu wa Mungu kwa utukufu wake pekee na heshima. Yeye kama shujaa, alishuka kutoka mbinguni, katika utimilivu wa wakati, na akashinda kupitia msalabani.

Na wote waliokombolewa wataishi kwa furaha milele.

Mwisho

Made with FlippingBook Digital Publishing Software