Theolojia Katika Picha
/ 4 9
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Hatua za Kuandaa Wengine Mch. Dkt. Don L. Davis
Hatua ya Kwanza
Kuwa Mwalimu katika hilo, ukijitahidi kufikia umahiri kwa kulifanya tena na tena, kwa ubora, na kwa furaha . Lazima ujifunze kulifanya, na kulifanya vizuri. Ingawa huhitaji kuwa mkamilifu, unapaswa kuwa na uwezo wa kulifanya, kufanya mara kwa mara, na kukua katika mazoezi yako ya kulifanya. Hii ndiyo kanuni ya msingi zaidi ya mchakato wa ulezi na ufuasishaji wowote. Huwezi kufundisha usichojua au usichoweza kufanya, maana ni lazima uzingatie ukweli kwamba Mwanafunzi wako anapokuwa amefunzwa kikamilifu, atakuwa kama wewe (Luka 6:40).
Hatua ya Pili
Chagua Mwanafunzi ambaye pia anatamani kukuza ustadi wa jambo hilo, anayefundishika, mwaminifu, na anayepatikana . Yesu aliwaita wale Thenashara wawe pamoja naye, na kuwatuma kuhubiri (Mk 3:14). Uhusiano wake ulikuwa wazi, haukuwa wenye mashaka au wa kulazimishwa. Nyajibu na majukumu ya uhusiano lazima yaelezwe kwa uangalifu, yajadiliwe vizuri, na kuwepo na makubaliano yaliyo wazi.
Hatua ya Tatu
Elekeza na uwe kielelezo cha kazi mbele ya Mwanafunzi wako ukiambatana naye . Anakuja karibu yako kusikiliza, kutazama na kufuatilia. Unaifanya tena na tena na kwa ustadi, na Mwanafunzi wako anakuja pamoja nawe ili kuona jinsi inavyofanyika. Picha ina thamani ya maneno elfu. Aina hii ya kutoa nafasi kwa mwanafunzi kutazama katika mazingira ya uhuru pasipo shinikizo lolote ni muhimu kwa mafunzo ya kina (2 Timotheo 2:2; Wafilipi 4:9).
Hatua ya Nne
Ifanye kazi hiyo na mfanye pamoja . Baada ya kumwelekeza mwanafunzi wako kwa vitendo kwa njia nyingi na mara nyingi, sasa unaweza kumwalika kushirikiana nawe kama mshirika katika mafunzo, mkifanya kazi pamoja. Lengo ni kufanya kazi pamoja, kuwa na uwajibikaji wa pamoja. Mnaratibu juhudi zenu, mkifanya kazi pamoja kwa maelewano ili kutekeleza shughuli hiyo.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software