Theolojia Katika Picha

5 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Hatua za Kuandaa Wengine (muendelezo)

Hatua ya Tano

Mwanafunzi wako anafanya kazi hiyo mwenyewe, mbele yako ukiambatana naye . Unatoa fursa kwa mwanafunzi wako kufanya mazoezi ya kazi hiyombele yako huku ukitazama na kusikiliza. Unajitolea kusaidia, lakini utoe msaada huo ukiwa nyuma yake na kumwacha awe mstari wa mbele; unatoa ushauri, mchango, na mwongozo pale anapohitaji, lakini yeye ndiye anayefanya kazi hiyo. Baadaye, unatathmini na kufafanua chochote ambacho unaweza kuwa umekiona katika mchakato huo (2 Wakorintho 11:1).

Hatua ya Sita

Mwanafunzi wako anafanya kazi hiyo peke yake, akiifanyia mazoezi mara kwa mara, kwa wepesi na ustadi hadi atakapofikia viwango vya umahiri mkubwa . Baada ya mwanafunzi wako kufanya kazi hiyo vyema chini ya usimamizi wako, yuko tayari kuachiliwa ili kuufanya ujuzi huo kuwa wa kwake kwa kujijengea mazoea ya kuutumia katika maishani yake. Wewe unakuwa mshirika mwenza wa mwanafunzi wako; wote wawili mnaweza kufanya kazi bila shuruti au msaada kutoka kwa mwingine. Lengo ni ujuzi na uzoefu katika kazi (Waebrania 5:11-15).

Hatua ya Saba

Mwanafunzi wako anakuwa mlezi wa wengine , akichagua wanafunzi wengine waaminifu ili kuwaandaa na kuwapa mafunzo . Mchakato wa mafunzo huzaa matunda pale ambapo mwanafunzi, akiwa amefahamu jambo ulilomwezesha kufanya, anakuwa mkufunzi wa wengine. Hiki ndicho kiini cha mchakato wa kufuasa na mafunzo (Waebrania 5:11-14; 2 Timotheo 2:2).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software