Theolojia Katika Picha

4 9 2 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Usomaji kuhusu Kuaminika kwa Kihistoria kwa Agano Jipya

Simulizi za Kihistoria kuhusu Yeshua: Ukweli au Hadithi za Kubuni?

Luka 1:1-4 - Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, 2 kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3 nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu , Theofilo mtukufu, 4 upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa. Yohana 20:30-31 - Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo , Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Yohana 21:24-25 - Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli . 25 Kuna namambomengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa. Inapokubaliwa kwamba kuna tofauti za maoni ndani ya Agano Jipya na kwamba kuna kutofautiana ndani ya simulizi za historia, wengi huhisi kwamba kuaminika kwa Agano Jipya kama hati ya kihistoria kunavunjwa au hata kubatilishwa . Uwazi unatuhitaji kukiri, bila kujali mtazamo wetu, kwamba maandiko ya Agano Jipya yanarekodi matukio ambayo yalitokea angalau kizazi kimoja kabla ya kuandikwa. Tunapoongeza juu ya hili maelezo ya Agano Jipya yanayowataja wanafunzi kama wasiojua kusoma na kuandika (Mdo. 4:13), lazima tukubali kwamba kulikuwa na hatua muhimu ya uwasilishaji wa mapokeo ya Yesu kwa mdomo kabla ya Injili kuandikwa kama tulivyo nazo leo . Tofauti zinazoonekana kati yao katika baadhi ya matukio si masuala ya kusababisha matatizo makubwa – kama vile uhakika wa kwamba familia ya Yesu iliishi hapo awali Bethlehemu (Mt. 2) au kama walikuwa huko kwa muda tu, lakini waliishi Nazareti (Luka 2). Hata hivyo, juhudi zozote makini za kulielewa Agano Jipya lazima zikubaliane na tofauti hizi na kutafuta kuzijibu. Mtazamo wa Uhakiki wa Kisasa Sehemu ya I: Kuaminika kwa Kihistoria kwa Agano Jipya ni Nini?

 Aya hizi zinaendana kwa sehemu kubwa na tafsiri ya David H. Stern, The Complete Jewish Bible

 Howard Clark Kee. Understanding the New Testament. Englewood Cliffs, NJ: Prentice-Hall, 1983. uk. 9.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software