Theolojia Katika Picha
/ 4 9 3
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Usomaji kuhusu Kuaminika kwa Kihistoria kwa Agano Jipya (muendelezo)
Mtazamo wa Uhakiki wa Kisasa Sehemu ya II: Je, Simulizi za Mateso ya Yesu ni Propaganda? Ni lazima pia tuhoji ikiwa inafaa kwetu kuweka, kama tuonavyo vema, viwango vyetu vya usahihi wa kihistoria kwenye hati kama Agano Jipya. Kama vile Yohana 20:31 anavyosema, yeye ameripoti simulizi ya matendo ya ajabu ya Yesu (“ishara”) ili “mpate kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Aliye Hai.” Ni wazi kwamba si wasomaji wake wote watafikia na kuamini mahitimisho yake, lakini yuko wazi katika kuwaambia wasomaji wake malengo yake. Na malengo hayo sio kuripoti tu mambo kama yalivyokuwa pasipo malengo mahusi au bila kutafuta matokeo fulani. Kwa kutumia neno hili katika maana yake ya msingi, yaani njia ya kueneza maoni au imani, Agano Jipya sio tu historia ya mambo kama yalivyokuwa, bali ni propaganda . Hata hivyo, historia katika wakati na utamaduni wowote daima ni maelezo kuhusu tukio pamoja na tafsiri yake; haiwezi kuwa maelezo tu ya matukio fulani pasipo malengo mahususi, kwa maana ya kukosa kabisa mfumo au mwelekeo fulani wa tafsiri au mtazamo. Kinachotakiwa ni kufahamu mawazo ya mwandishi, malengo ya maandishi, na kile ambacho kinamaanishwa katika misemo yake, mtindo wa uandishi na uwasilishaji, na lugha dhahania iliyotumika. Mtazamo wa Uhakiki wa Kisasa Sehemu ya III: Je, Mahitaji ya Jamii Ndiyo Yaliyoamua Ujumbe? Yesu wa Nazareti ndiye msingi wa kihistoria wa madai ya Wakristo kuwa jumuiya ya agano jipya. Hata hivyo, kama tulivyoona, uthibitisho wetu wa maandishi kumhusu uliandikwa muda mrefu baada ya kifo chake, labda katika nusu ya mwisho ya karne ya kwanza. Rekodi zetu ni mfululizo wa namna wale waliomwona Yesu kuwa ni Mjumbe wa Mungu walivyoitikia ufunuo huo, si ripoti za watazamaji waliotazama kwa mbali. Katika mchakato wa kuchambua hati hizi za imani tunajifunza juu ya Yesu, lakini pia tunajifunza juu ya jamii ambamo mapokeo kumhusu yalithaminiwa na kurithishwa kwa vizazi vya jamii husika . Kifo cha Kristo chenyewe kilihusishwa na Pasaka katika makanisa ya Paulo (1 Kor. 5:7); na katika jamii ya Yohana [yaani, katika makanisa ya Yohana], Yesu alichukuliwa kama Mwana-Kondoo wa Mungu (Yoh. 1:29; Ufu. 5).... Lakini ni Marko peke yake aliyetosheka kuthibitisha tu kwamba kifo cha Yesu kilikuwa cha lazima, bila kueleza kwa nini au jinsi gani, kwa hiyo anasema tu kwamba kifo cha Yesu ni kwa ajili ya wengine. Hivi ndivyo jamii ya Marko inavyosherehekea katika ushirika, huku wakitarajia kukamilika kwa idadi ya wateule katika enzi mpya.
Howard Clark Kee. Understanding the New Testament. Englewood Cliffs, NJ: Prentice-Hall, 1983. uk. 9.
Howard Clark Kee. Understanding the New Testament. Englewood Cliffs, NJ: Prentice-Hall, 1983. uk. 78, 121.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software