Theolojia Katika Picha
4 9 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Usomaji kuhusu Taipolojia Mch. Dkt. Don L. Davis
Ufahamu wa Vivuli Muhimu kwa Uelewa wa Kina wa Agano Jipya
Kuna vifungu vingi katika Agano Jipya ambavyo hatuwezi kuvielewa bila kufahamu kwa kiasi fulani vivuli hivyo. Waraka mzima kwa Waebrania karibu umeundwa na marejeo ya Agano la Kale: kama kiini, Kristo, amethibitishwa kuwa bora kuliko vivuli – bora kuliko Musa, kuliko Yoshua, kuliko Ibrahimu, kuliko Haruni, kuliko Hema ya kwanza, kuliko dhabihu za Walawi, kuliko wingu zima la mashahidi katika ukumbi wa picha wa imani; na mwisho, damu yake imethibitishwa kuwa bora kuliko damu ya Habili. Wakati fulani tunasahau kwamba waandishi wa Agano Jipya walikuwa wanafunzi wa Agano la Kale ; kwamba AK lilikuwa Biblia yao , na kwamba kwa kawaida walirejelea tena na tena mifano na vivuli vya AK, wakitarajia wasomaji wao pia kuvifahamu. Tukishindwa kuona madokezo haya, tunapoteza uzuri mwingi wa kifungu, na hatuwezi kukielewa ipasavyo . . . . [Ufahamu wa vivuli] hutupatia kiuasumu chenye uhakika cha sumu ya kile kinachoitwa “uhakiki wa hali ya juu zaidi.” Ikiwa tunatambua nia ya Kiungu ya kila kipengele cha kivuli, ingawa tunaweza tusielewe mafundisho yake yote, na ikiwa tunaamini kuwa kuna somo katika kila tukio lililorekodiwa, mashambulizi ya ukosoaji wa kisasa hayatatudhuru. Huenda tusifahamu kwa uwazi vya kutosha kuweza kuelewa kile ambacho wakosoaji wanasema, au namna ya kujibu shutuma zao; lakini ikiwa macho yetu yamefumbuliwa kuona uzuri wa vivuli hivyo, mashaka ambayo waandishi kama hao wanayaonyesha hayatatusumbua, na tutakuwa na kazi yenye faida zaidi kuliko kusoma kazi zao . Wakati ukosoaji mwingi sana huu wa uharibifu unaenea, hatuwezi kufanya vizuri zaidi ya kuwahimiza wote – hata Wakristo wachanga zaidi – kupata maarifa ya kibiblia kuhusu vivuli vilivyomo katika Neno la Mungu; maana ijapokuwa mambo haya amewaficha wenye hekima na akili, amewafunulia watoto wachanga . Je, Katika Nyakati Zetu Tunajifunza Biblia kwa Njia Ile ile na kwa Mbinu Zile zile kama Bwana na Mitume? Baada ya zaidi ya miaka ishirini ya kufundisha hemenetiki ya kisarufi-historia, naweza kuona tatizo moja tu kuhusiana nayo: haionekani kuendana na jinsi waandishi wa Biblia walivyofanya siku zote! Tunapochunguza jinsi waandishi wa Biblia walivyotumia Maandiko yaliyoandikwa hapo awali, tunaona kwamba walionekana “kugundua” maana hapo ambayo, kwa kuzingatia muktadha wake wa asili, haiwezi kufikiriwa kwamba ilikuwepo katika akili ya mwandishi wa kwanza. Suala hili linaonekana hasa katika
Ada R. Habershon, Study of the Types . Grand Rapids: Kregel Publishing, (1957) 1974. uk. 19, 21
James DeYoung na Sarah Hurty, Beyond the Obvious . Gresham, OR: Vision House Publishing, 1995. uk. 24
Made with FlippingBook Digital Publishing Software