Theolojia Katika Picha
/ 4 9 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Usomaji kuhusu Taipolojia (muendelezo)
namna waandishi wa Agano Jipya walivyotumia vifungu vya Agano la Kale kuthibitisha kwamba Yesu Kristo alitimiza unabii (au kueleza jambo fulani la kitheolojia.)
Je, Tunaweza au Tunapaswa Kurejesha Ufafanuzi wa Agano Jipya?
Kuhusu swali kama tunaweza kurejesha ufafanuzi wa Agano Jipya, S. L. Johnson anajibu: “Bila kusita jibu ni ndiyo, ingawa haturuhusiwi kuyapa matokeo ya kazi na juhudi zetu sifa ya kutokosea kama Bwana na Mitume wake. Wao ni waalimu wa kutegemewa wa mafundisho ya Biblia na ni waalimu wa kutegemewa wa hemenetiki na ufafanuzi. Si tu kwamba tunaweza kurejesha mbinu zao za ufafanuzi, ukweli ni kwamba tunapaswa kuzirejesha ikiwa tunahitaji tufundishwe ufahamu wao wa Maandiko.” Vipi kuhusu Taipolojia kama Mbinu Sahihi na Muhimu ya Ufafanuzi wa Biblia? [Taipolojia] ni mbinu nzuri na imetumiwa sana katika Agano Jipya. Kwa mfano, samani za hema la kukutania na mambo mengine yanayohusiana nayo na hekalu (madhabahu na dhabihu, pazia, kifuniko cha dhahabu cha sanduku la agano) vyote ni vivuli vya Kristo na vya mambo ya mbinguni (ona Ebr. 9). Tunapokuja kwenye taipolojia, lazima tuepuke kuwa na mtazamo mpana sana au mfinyu sana katika tafsiri yetu. Tunakuwa wenye mtazamo mpana sana ikiwa tutatumia taipolojia kila mahali. Tunaweza kuwa na mtazamo mfinyu sana ikiwa tutaikataa taipolojia kama mbinu ya ufafanuzi kwa msingi wa dai la kwamba haipatani na maana halisi na iliyo wazi, inayopatikana kwa njia ya utafiti wa kisarufi-historia. . . . Bado tunaamini kwamba taipolojia haipaswi kutenganishwa na ufafanuzi wa Maandiko, ingawa haiwezi “kudhibitiwa kihemenetiki, lakini inafanyika katika uhuru wa Roho Mtakatifu.” Inahusisha sana maana ya ndani zaidi na ilitumika pasipo tatizo ndani ya Biblia kama mojawapo ya mbinu zake za ufafanuzi ( ona 1 Kor. 10; Rum. 5).
James DeYoung na Sarah Hurty, Beyond the Obvious . uk. 265
James DeYoung na Sarah Hurty, Beyond the Obvious . uk. 74
Matumizi Mbalimbali ya Neno Typos katika Agano Jipya
Kwa namna ambavyo Maandiko yanatumia lugha ambayo kimsingi ilikuwa ya kawaida kwa watu wa nyakati zake, matumizi yake ya maneno fualni kimsingi yamefanyika katika uhuru wa kitumia aina mbalimbali za fasihi ambazo zilizoeleka kutumika katika usemi wa kawaida wa watu; na ni mara chache sana inatokea kwamba maneno yanatumika,
Patrick Fairbairn, Typology of Scripture . Grand Rapids: Kregel Publishing. uk. 42
Made with FlippingBook Digital Publishing Software